Heche: Kabudi na Kitila walijulikana kwa kupiga kelele vyuoni, Kaijage amekamatwa Wahadhiri wako kimya!

Heche: Kabudi na Kitila walijulikana kwa kupiga kelele vyuoni, Kaijage amekamatwa Wahadhiri wako kimya!

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amewajia juu wanataaluma na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kwa kuendelea na masomo kama kawaida wakati mwenzao, Mhadhiri Melkisedeki Kaijage wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akishikiliwa na vyombo vya dola kwa kutumia uhuru wake wa fikra.

Heche amekosoa kimya hicho akitaja kuwa ni utamaduni hatari unaohatarisha uhuru wa taaluma, huku akimnukuu mchungaji wa Ujerumani, Martin Niemöller, kukumbusha madhara ya kutotetea haki za wengine pale wanapokandamizwa na utawala.


Soma kuhusu sakata la Mhadhiri wa Chuo Kikuu UDOM
 
Kipindi Moi anafuta vyama vya siasa na mikutano ya siasa Kenya , jukwaa pekee lililobaki kwa watu kutoa maoni na kufanya mijadala lilibaki ni vyuoni kupitia wahadhiri na wanafunzi .

Hata hatua ya Moi kufikia kushindwa na kukubali masharti ya kurudisha vyama vingi mageuzi yalianzia vyuoni.
 
Enzi hizo Kabudi akiwa Mhadhiri wa sheria UDSM, huko Zanzibar kulikuwa na kiongozi anaitwa Comandoo. Bifu lililotokea. Nilipenda msimamo na hoja za Kabudi yule.

Bw Comandoo aliwasweka ndani viongozi wa uoinzani wakiongozwa na Maalim Seid kwa kilichoelezwa kuwa ni Uhaini.

UDASA ya akina kabudi, tena akiwa msemaji mkuu, alipinga hadharani kuwa kosa la uhaini haliwezi kufanyika Zanzibar kwani Zanzibar sio nchi.

Comandoo alikuja juu kwa mikwara mingi, Yule Kabudi wa ukweli, alimjibu kuwa, kwa mujibu wa mkataba wa Montevideo wa mwaka 1930', ili nchi iwe na hadhi ya kuwa nchi, ni lazima iwe na Jeshi huku kiongozi wake akihudhuria UNGA, Akaulizwa Comandoo, Zanzibar ina sifa hizo?

Akaambiwa, ( kama nakumbuka vyema), hadhi yako ni sawa na Makamba( aliyekuwa RC wa Dar)enzi hizo. Kesi hiyo baadaye ilifutwa kwa misingi hiyo. ( kama kumbukumbu zangu ziko sawa kwa story hii).
Huyo ndio Kabudi kabla ya kutoika jalalani. Tena wako wengi wengine ni pamoja na yule wa mipango, Bashir nk.
Kama alivyosema Ulimwengu vyuo vyetu vikuu kwa sasa ni Sekondari zilizochangamka. Hakuna hata Jumuiya za wasomi.
 
Mimi nitashangaa sana kama wahadhiri hawataitisha mgomo kugoma huu uhuni unaotaka kupandikizwa vyuoni.
"...uhuni unaotaka kupandikizwa vyuoni"?

Kuna uhuni hadi ndani ya Jeshi linaloitwa la "Wananchi wa Tanzania", sembuse huko vyuo vikuu?

Kuna sehemu gani nyingine ndani ya nchi hii ambako "uhuni haujapandikizwa", labda mbali ya CHADEMA, ambayo ndiyo pekee inayoendelea kupigwa ikubali uhuni.
 
Kipindi Moi anafuta vyama vya siasa na mikutano ya siasa Kenya , jukwaa pekee lililobaki kwa watu kutoa maoni na kufanya mijadala lilibaki ni vyuoni kupitia wahadhiri na wanafunzi .

Hata hatua ya Moi kufikia kushindwa na kukubali masharti ya kurudisha vyama vingi mageuzi yalianzia vyuoni.
Kuna jambo la kipekee sana limewapata waTanzania. Napata shida sana kuelewa imekuwakuwaje hadi tukafikia kwenye hatua duni kama tuliyo nayo sasa hivi.

Huu mfano wa waTanzania kuuliwa kikatili kabisa umetuingia ndani kabisa, hata kutamka tu maneno ya kupinga uovu linakuwa tatizo?.
Kila mtu analinda kwake, asipate madhara!
 
Nakumbuka back in 2009/2010 pale Udsm by then Dr Kitila Mkumbo alikua anatufundisha course moja inaitwa SOCIAL PSYCHOLOGY,.. jamaa alikua anatulisha madini kuhusu saikolojia ya binadamu including wanasiasa, aisee ilikua good moment sana...

Mnaenda zenu Nkurumah pale mnasikiliza nondo za akina Palamagamba Kabudi, Dr Lwaitama, Dr Mvungi, Dr Bashiru Ally... Ilikua ni nondo mwanzo mwisho..

Yaani ile UDASA ilikua generation moja tamu, Dr Mkumbo ni moja ya watu walionipa conscious sana... Siku hizi nikimwangalia mpaka nachoka, wale jamaa zangu tuliofundishwa nae huwa tunapigiana simu hatuamini macho yetu.
 
Back
Top Bottom