DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amesema chama hicho kimepoteza kiongozi muhimu kufuatia kifo cha muasisi wake, Mzee Edwin Mtei.
Akizungumza wakati wa salamu za chama katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu.
Heche amesema CHADEMA kinatoa salamu za pole kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, ambaye kwa sasa yupo mahabusu akikabiliwa na kesi alizozitaja kuwa ni za uongo.
Amesema chama hicho kinathamini sana mchango wa Mzee Mtei katika kujenga misingi imara ya uongozi wa kimaadili, akiwashukuru Zitto Kabwe pamoja na Baba Askofu kwa maelezo yao kuhusu msimamo na maamuzi aliyokuwa akiyafanya marehemu katika uongozi wa Taifa.
Ameeleza kuwa Mzee Mtei aliwahi kuacha nafasi ya Uwaziri wa Fedha baada ya kutofautiana kimtazamo na Rais wa wakati huo, akibainisha kuwa si jambo rahisi kwa kiongozi kuacha madaraka ya juu kwa misingi ya msimamo na taaluma.
Kwa mujibu wa Heche, CHADEMA itaendelea kumkumbuka Mzee Mtei kama mfano wa kiongozi aliyesimamia misingi, akiongeza kuwa katika mazingira ya sasa, mtu anayetoa hoja tofauti huonekana kupotezwa, hali inayotokana na kuendelea kushikilia misimamo aliyoyaacha marehemu Mtei.