PreGE2025 Heche: Nimepata taarifa kuwa kuna mpango wa kunikamata wakati wowote kuanzia sasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwani kampeni zimeanza? Unajua maana ya UASI??;
 
Kushiriki au kutokushiriki uchaguzi ni HAKI ya kila Mtanzania. Kama inaruhusiwa kuhamasisha kushiriki, basi ni halali vilevile kuhamasisha kutokushiriki. Kama Ccm inapinga Reforms na haichukuliwi hatua, kwanini Chadema wasumbuliwe kwa kusisitiza Reforms?
 
Kama unavunja Sheria unapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua bila huruma
 
"NO REFORM, NO ELECTION", ni mbegu iliyokwisha ota na kumwagiliwa maji ikue na kukomaa. Hakuna yeyote wa kuizuia mbegu hiyo sasa iliyomo mioyoni mwa watu.

Ukijaribu kuing'oa, ni wewe utakayengooka!
 
Anahangaika tu
 
Tume ya Haki za Binadamu Tanzania, Human Right Watch watoe ulinza haraka kunusuru maisha ya hawa Wazalendo
 
Hakuna kuogopa wala kurudi nyuma💪🏿🔨📌
 
Nawaonea huruma viongozi wa chadema kujitoa kwa watu wasio wathamini maana ni kama raia wanaona ni sawa tu,hawa viongozi wanateseka sana
 
Kama huogopi kukamatwa kelele za nini?
Zakayo mfupi. Una akili fupi kama jina lako. Na wewe ni great thinker?
Unajua gharama za kulaza mgonjwa muhimbili ni elfu 50 kwa siku?
Ulishawahi kusikia ccm wakilitamka hilo pipote?
 
CCM wana polisi, jeshi, usalama wa CCM, Tume ya Uchaguzi iliyojaa mashushushu, maDED, maDC, majority ya Majaji etc etc lakini bado wana ushamba wa kukamata watu na kuwapatia kesi za mchongo?

Wananchi wengi wamechoshwa na madudu na turn up kwenye mikutano ya CHADEMA ni ishara tosha. Kukamata viongozi wa upinzani sio solution ya kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…