Mimi na Hamida tumetoka mbali sana! Ananijuwa vizuri tabia zangu na hata nikidanganya anajuwa na hugeuka mbogo bora umwambie ukweli huwa anatulia. Kama kununa atanuna, ama atalia lakini huwa afadhali kuliko ukimdanganya kesi yake huwa haiishi!
Tu wazee sasa! Hakuna pilikapilika na hata huko nyuma baada ya kumuoa nilibadilika na kuwa mume bora sana.
Ajali katikati hapa ni chache sana, lakini nimeamua kuleta simulizi hii maana sasa uzeeni naona ni hekaheka tu.
Endelea kufuatilia utaelewa tu, Hamida alikuwa na mpango wake wa siri....
Ooops, nitamaliza utamu.