Hekima, busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni

Hekima, busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
MADA YA LEO: NI MUHIMU SANA MTU KUWA NA NIDHAMU YA KULA KWA STAHA MBELE YA WATU (KADAMNASI)

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi. Kila siku tukikaa kujadili masuala ya wazungu ni nani atazungumzia ustaarabu wetu?

Ndugu zangu wa Tanzania;

Miezi kadhaa iliyopita nilipata kuhudhuria sherehe moja ya harusi ya mtoto wa kike wa ndugu yangu wa karibu sana iliyofanyika katika ukumbi fulani maarufu sana kule mkoani Arusha. Kusema ukweli wa Mungu harusi ile ilifana sana. Ndugu, jamaa na marafiki sote tulijumuika tukala na kufurahi kwa pamoja.

Tulipiga story mbalimbali pamoja na kukumbushana mambo ya zamani kwa maana ilikuwa ni fursa pia ya kuonana na watu ambao hatukuweza kuonana kwa muda mrefu sana. Sasa kama inavyofahamika na wengi kwamba sherehe huwa ni ratiba mahususi na ratiba ile huwa ina vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na kuwapokea maharusi, kutambulishana, kwenda kuchukua chakula pamoja na utoaji wa zawadi.

Hapa kwenye uchukuaji wa chakula ndio mada kuu ya mjadala kwa siku ya leo. Muda wa chakula ulipowadia ndugu mshereheshaji (MC) aliwaita maharusi kwanza, kisha wakafuata wazazi wa pande zote mbili na kumalizia na sisi akina Infantry Soldier (Kwa maana mimi kudandia sherehe ni kama ulimi na mate hahahaaaaaa I am joking....!!!!!!)

Bwana harusi alikuwa ni mtoto wa kiongozi fulani huko na yeye binafsi alikuwa anafanya kazi katika NGO moja kubwa tu huku Dar, hivyo ile sherehe ilikuwa ni ya budget kubwa kiasi. Hakika chakula kile kilikuwa ni kitamu sana sana tena saaaaana.

Kila mtu alikula na kufurahi lakini cha ajabu MC yule yule akatangaza kwa mara kadhaa kwamba ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana, CHAKULA BADO KIMEBAKI KINGI TU KWA ANAYETAKA KUONGEZA RUKSAAA hahahaaaaaa hapa ndio kasheshe ilipokuwapo. Amini usiamini, hakuna aliyethubutu hata kusimama kwenda kuongeza msosi isipokuwa jamaa fulani 3 ambao ni rafiki wa bwana harusi.

Kile kitendo walikifanya wao lakini aibu niliiona mimi. Inakuwaje mtu mzima na ndevu zake anashindwa kuizuia tamaa ya muda mfupi na kuamua kujidhalilisha namna ile mbele ya kadamnsi?

Sasa ndio nikajawa na maswaki mengi kuliko majibu kwamba;

Je, unafikiri ni jambo sahihi na busara mtu kukosa Busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni?

USISAHAU
: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

MAONI YA MDAU
=======
Arusi zilizostaarabika,huwa msosi ukiishaandaliwa hutolewa tangazo kwenda kujisevia mtu kipimo anachotaka.

Kunakuwa na msimazi tu ambaye hagawi, kazi yake ni kuangalia usalama wa vyombo na vyakula, kazi ya kujipakulia ni ya kila mtu kujikadiria atakavyo yeye.

Na huku kwenye vinywaji ni mwendo wa coctail tu, vinywaji kujazwa mezani na kuzibuliwa vizibo kabisa ili kila mtu anywe atakacho, bia iwe soda nk nk achague mwenyewe.

'Gage' ya ustarabu hupanda sana kadri mtu anapopewa uhuru wa kujisevia na si kugawiwa.

Kumekuwa na uchoyo kwa waandaaji na wahudumu.

Mtu kachangishwa 'malaki', akija kwenye msosi mgawaji anagawa kwa kusuasua hakandamizi kamusi sawasawa likasheheni zaga, mtu anaondoka kwenye vyakula kwenda kukaa kula hajaridhika.

Tukija kwenye vinywaji napo, mtu anakaukiwa chupa na akinyoosha mkono ahudumiwe, wahudumu wanajifanya hawaoni na muda unakwenda ili vinywaji vibakie!

Uchoyo uchoyo tu huku watu wamechangishwa matrilioni haufai.

Kama kuna mpangilio mzuri na management iliyokwenda shule, hatuwezi kuja na topic kama hizi sijui za kuona aibu mtu kula, huo ni udwanzi tu unaofanywa na waandaaji ili harusi inapomalizika wabakie na 'faida'!
 
Usiseme watanzania hatuongezi msosi. Labda nyie wa kishua, uku uswazi wamama wanaondoka naubwabwa kwenye pochi zao, watoto wanaweka ubwabwa kwenye mashati.

Ok let's get it serious. Wewe ushasema mulikuwa mnajisevia wenyewe Sasa si mlijikadiria vya kuwatosha? Utaongeza vp wakati umetosheka mkuu.
 
Back
Top Bottom