Hekima: Usitoe sana sadaka bila kujibakiza, tumia akili sana, uliza moyo wako, angalia watoto na familia, angalia nguo na viatu vyako ndio utoe sadaka

Hekima: Usitoe sana sadaka bila kujibakiza, tumia akili sana, uliza moyo wako, angalia watoto na familia, angalia nguo na viatu vyako ndio utoe sadaka

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2012
Posts
2,977
Reaction score
1,897
Hapo zamani tulikuwa na wazungu walitufundisha kuwa Mungu huwasaidia watu wanaojisaidia wenyewe.

Hawa wazungu walimaanisha ukifanyakazi kwa bidii na kumtumainia Mungu ndio utafanikiwa. Nimekutana na waumini flani wanatoa sadaka hadi wanakosa nauli ya kurudi nyumbani.

Niliwahi kuona mke wa mtu alitoa sadaka malimbuko hadi laki 5 wakati wanaishi Maisha ya kuhangaika mpaka Leo.

Kuna baadhi ya makanisa wanasadaka hadi tano kwa Jumapili Moja.
Ndugu yangu kipato unachopata unapata kwa jasho sana na kulala hoi. Usikitawanye kwa kufuata mkumbo.
Muulize Mungu na moyo wako umtolee kiasi gani.Si lazima utoe kila sadaka kaa kwenye kiti wakati huo Sali kimoyo moyo soma biblia.
Unatakiwa ujipende nunua nguo nzuri, weka akiba ya baadae.

Mwili wako ni hekalu la Mungu litunze kwa upendo na shukurani.
Hakuna padri mchafu mchafu wala shehe machafu mchafu.
Waumini ndio wanaokuwa wa chafu wa chafu. Vunjeni kabati kila siku laleni pazuri. Kuna waumini Safi wanatoa sadaka sana lakini ukienda kwao unashangaa. Jipendeni.
 
Huendi mbinguni kwa kutoa sadaka, na wala usipotoa siyo kuwa hutaenda mbinguni.

10% ya kila unachokipata, ni ya Mungu.

Na hiyo ya Mungu, siyo kanisani tu unaweza kutoa kwa maskini wajane na yatima. Makanisa yamekengeuka na kuijiwa na tamaa ya fedha na kugeuza waumini kama mradi wao.
 
Back
Top Bottom