DOKEZO Hela za kujikimu kwa waajiriwa wapya ziko wapi 2022

DOKEZO Hela za kujikimu kwa waajiriwa wapya ziko wapi 2022

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Lil bees

Senior Member
Joined
May 17, 2022
Posts
143
Reaction score
158
Wakuu uzima upo kwenu?

Leo niseme kero tuliyo nayo waajiriwa wapya wa ajira za afya kwa mwaka 2022. Viongozi wetu mbona hatuwaelewi inakuaje mtu aliye pangwa kituo cha kazi toka mwezi wa 6 mpaka leo hajapewa pesa ya kujikimu?

Kuna mikoa kama Kagera kuna wilaya bado hatujapewa hela za kujikimu, kuna mkoa wa mara na halimashauri zake hawajapewa pesa za kujikimu. Hili lina tupa picha ya jinsi msivyo jali wafanyakazi. Mtu anaripoti mwezi wa 6 halafu mpaka mwezi wa 9 huu hajapewa hela za kujikimu. Nimetaja mikoa miwili ninayojua kuwa bado hawajapewa hela za kujikimu. Kagera na Mara. Kuhusu halmashauri ni zote hasa za pembeni. Kwa mara ni halimashauri ya Butiama na Musoma Vijijini bado.

Waziri wa TAMISEMI, Bashungwa fanyeni haraka watu wapewe pesa hizo. Mlisema tukipata changamoto zozote tusisite kuwa taarifu hizi ndizo taarifa sasa zipokeeni na zifanyieni kazi.

La muhimu zaidi.
Kama wapo wakubwa Serikalini humu mnajua ID zao wa-tag wote waone huu uzi. Habari ziwafikie. Mnawanyanyasa hawa waajiriwa wenu na ni kila mwaka kwa maelezo ya wazoefu kazini. Kwanini haya mambo yanajirudia?
 
Wakuu uzima upo kwenu.?

Leo niseme kero tuliyo nayo waajiriwa wapya wa ajira za afya kwa mwaka 2022. Viongozi wetu mbona hatuwaelewi inakuaje mtu aliye pangwa kituo cha kazi toka mwezi wa 6 mpaka leo hajapewa pesa ya kujikimu.?

Kuna mikoa kama kagera kuna wilaya bado hatujapewa hela za kujikimu, kuna mkoa wa mara na halimashauri zake hawajapewa pesa za kujikimu. Hili lina tupa picha ya jinsi msivyo jali wafanyakazi. Mtu anaripoti mwezi wa 6 afu mpaka mwezi wa 9 huu hajapewa hela za kujikimu. Nimetaja mikoa miwili ninayo jua kuwa bado hawajapewa hela za kujikimu. Kagera na Mara. Kuhusu halimashauri ni zote hasa za pembeni. Kwa mara ni halimashauri ya butiama na musoma vijijini bado.
Yaani hamlipwi mishahara au?au hizo shekel za kujikimu ni nje ya salary?
Kama ni nje,Bora zifutwe,posho,pesa za safari,
 
Mkuu embu nieleweshe hapa

Hawajapewa hela ya kujikimu ukimaanisha mshahara au kuna mshahara na pesa ya kujikimu pembeni ila mshahara wanapata
Mshahara ni malipo ya mwezi kwa muajiriwa na hela ya kujikimu ni pesa unayopewa ya kuanzia maisha kituoni kwako kabla mshahara haujakufikia. Sasa jiulize tumekaa miezi miwili kazini ila.mshahara nao mwezi ule wa 7 hatukupewa tumelipwa mwezi wa 8 hiyo wengibtulikua likizo ya sensa afu umepangwa mbali hela imeishia kwenye nauli na madeni tumerudi vituo vya kazi hakuna hela za kujikimu bado. Sijui ni 80000 au 100000 kwa mara 7 na nauli ulizotumia wanasema unarudishiwa
 
Wakuu kama.mpo zaidi mnaoijua mikoa au halimashauri ambazo bado njooni mtaje zote kwa uzi wangu huu. Uwafikie walengwa
 
Hata mm namjua dogo mmoja ni mwalimu mpya wilaya ya Mkalama,Singida analia njaa sana.
Wapeni pesa zao kama mmeshindwa waambieni warudi makwao wakalime na kufuga.

Mnachangia mabinti wa kike kunyanduliwa bila breki.
Kweli hili. Chukulia maadam hana kitanda wala pakulala maana hz hela hatuja pewa akakaribishwa geto kwa mtu kujistiri ana achwa kweli
 
Mshahara ni malipo ya mwezi kwa muajiriwa na hela ya kujikimu ni pesa unayopewa ya kuanzia maisha kituoni kwako kabla mshahara haujakufikia. Sasa jiulize tumekaa miezi miwili kazini ila.mshahara nao mwezi ule wa 7 hatukupewa tumelipwa mwezi wa 8 hiyo wengibtulikua likizo ya sensa afu umepangwa mbali hela imeishia kwenye nauli na madeni tumerudi vituo vya kazi hakuna hela za kujikimu bado. Sijui ni 80000 au 100000 kwa mara 7 na nauli ulizotumia wanasema unarudishiwa
Hua jumla ni shilingi ngapi mnapewa mkuu
 
Hua jumla ni shilingi ngapi mnapewa mkuu
Hawa wazoefu wanatuambia inatofautiana kwa halimashauri wanasema mfano waliopo mjini inakua kubwa kuliko waliopo halimashauri za pembeni ya miji na majiji. Exactly sijajua ni kiasi gani nahisi his tu wanavyosema kama 80k mara 7 wengine 100k mara 7 hivyo hapo sipaelewi
 
Kuna maeneo washapewa leo na jana hizo hela za kujikimu ila kuna wadau wangu wa singida na butiama na musoma vijijini wanasema hawaja pewa bado hizo hela wana lalamika. Tupeni bwana hela zetu tuna maisha magumu nyiie vipi.
 
Back
Top Bottom