Hela zimesharudi mtaani?

Hata kama mtu unapesa hauwezi kukubali kuranguliwa.

Ukitaka kujua pesa ipo mtaani au lah basi angalia kasi ya ujenzi , idadi ya watu kwenye shopping malls /super markets /local markets etc
 


Two wrongs don't make a right - Kubutua kwa Maza hakumsafishi JIWE.
 
Kuziona fedha mtaani huwezi kuziona kama unavyoona chupa za maji zilizotumika au karatasi. Bali yafuatayo ndiyo kisababishi;

1. Serikali ikilipa madeni ya ndani (local creditors). Kumbuka Mwendazake alisema anakakiki madeni ya ndani na akawa halipi. Wanaoidai Serikali wakilipwa nao watawalipa wanaowadai.

2. Mabenki kuongeza kasi ya kukopesha fedha kwa wenye miradi. Wakati wa Mwendazake Mabenki yalipunguza Imani kwa wakopaji kwa kuwa Serikali ilikuwa inaweza kuwanyang'anya fedha wakati wowote.

3. Wenye fedha kuzipeleka Benki. Watu wengi waliwekwa nje ya nchi na wengine walichimbia chini fedha kwa kuwa Serikali ya Mwendazake ilikuwa inaweza kuangalia akaunti ya mtu na kumfungulia mashtaka au kuzinyang'anya.

4. Wawekezaji wa nje wanapoanzisha miradi. Wakati wa Mwendazake hakukuwa na miradi mipya ambayo ingetengeneza ajira.

5. Kukuza biashara ya nje. Biashara ya mahindi na mbao kwenda Kenya ilikuwa imesimama. Kwa hatua za kuruhusu biashara mipakani mzunguko utaendelea.

6. Mwananchi mwenyewe kujihusisha na uzalishaji mali/ huduma kwa kuwa hakuna mtu anagawa fedha mtaani.

Katika hayo siyo rahisi kuyaona katika kipindi cha mwezi mmoja bali ni kipindi cha miezi 9 hadi mwaka.
 
Hata kama mtu unapesa hauwezi kukubali kuranguliwa.

Ukitaka kujua pesa ipo mtaani au lah basi angalia kasi ya ujenzi , idadi ya watu kwenye shopping malls /super markets /local markets etc
Watu walipunguza kwenda magengeni wakati wa Magufuli?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Watu walipunguza kwenda magengeni wakati wa Magufuli?

Enzi za jiwe malalamiko fedha hakuna yalikuwa mengi sana ukilinganisha na sasa , mimi ni fundi ujenzi ,nimejaribu kufanya mizunguko sehemu mbali mbali ,watu wameanza kujenga sana maybe inachangiwa na serikali kupeleka huduma za kijamii hivyo mtu anaona bora ajenge aachane na kupanga!
 
Zirudi wapi. Soon wataanza kumkumbuka Magufuli wasimpate. Hakuna taifa lenye fedha mitaani zaidi ya uvivu na ukosefu wa ubunifu.
 
Huu uongo sijui unasaidia nini
 
Sijui maana alishanipiga block kitambo , imagine mtu anatembeza block kwasababu ya hoja kinzani hapo hawezi kuamrisha Polisi! Hilo sikutegemea kabisa kwa mtu wa aina yake! Baada ya hapo nikala [emoji724] ya Jasusi Chahali [emoji38]
Wanaharakati wanapiga block sio mchezo, kupinga hoja yake ni tusi kwake.

Alafu wanataka uhuru wa kujieleza. Wapumbavu sana wale watu.
 
Hela zipo angalau watu sasa wanajenga, nendeni site huko mkaone mijengo ya maana, we kutwa upo mtandaoni kuanzisha vi thred uchwara utabaki kama ulivyo kuwa chawa tu,

Mama anaupiga mwingi
Hili la ujenzi upo sahihi kabisa. Mafundi ujenzi wengi walihamia kwenye kuendesha bodaboda....

Hivi sasa sura zao zinaota nuru...
 
Waliotupumbaza kumpinga JPM na harakati zake kwa mazingira yanavyoonekana wanakutana na hela ila sisi pangu pakavu mazingira yamekuwa magumu zaidi kuliko awali maana jamaa wanataka kufidia hasara ya miaka 6 ndani ya muda mfupi.
JPM angevumiliwa walau miaka 5 tena nchi ingebadilika walau kwa asilimia kadhaa kuliko sasa ambapo tunarudi nyuma kwa kasi.
Tulidanganywa na siasa uchwara za mitandaoni tukamkatisha tamaa jpm.
Kauli ya jpm kuwa matajiri wataishi kama mashetani ilimaanisha matajiri wetu wengi ni wezi hivyo alikuwa anaitaka pesa ya umma kufanyia shughuli za umma.
Hakika tulimuelewa vibaya yule mzee.
 
Niliona hicho alichosema Mwigulu!

The guy is an idiot.
 
Reactions: BAK
πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ‘πŸ½
Niliona hicho alichosema Mwigulu!

The guy is an idiot.
 
Huu uongo sijui unasaidia nini

Uongo gani Mkuu? Watu wengi wanajenga sana mkuu ,sehemu nazopitaga serikali inaweka miundombinu ya maji ,umeme na barabara kwa kasi kubwa sana! Enzi zetu tunakua maji tulikuwa tunafata zaidi ya 6km ila sasa maji yapo sebuleni,yapo washroom etc.

2016-2018 watu walikuwa hawajengi ,mafundi wengi tulipiga mihayo.
 
Malalamiko ya watu si lazima yaakisi uhalisia wa mambo.

Wengine kulalama ni jadi yao tu hata iweje.
 
Big up mkuu..na jiwe pia ikumbukwe hakuajiri..so kuongeza hata lower to middle income peoples hakukufanyika kwa kipindi chake..huku nako kunapafanya mtaani kuwe pagumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…