Hela zimesharudi mtaani?

Hela zimesharudi mtaani?

Moja ya malalamiko ya kipumbavu kabisa yaliyokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli ni kuwa eti hela hazikuwepo mtaani.

Sijui ni lini hasa Tanzania hii ambapo hela zilikuwepo bwerere mtaani! Kwa sababu, Tanzania ni nchi maskini. Ni nchi ya ulimwengu wa tatu.

Vipato vya wananchi wake ni vya chini sana. Si nchi nyingi ambazo nchi yetu imezipita kwa vipato vya wananchi.

Na tumekuwa nchi ambayo wananchi wake ni wa kipato cha chini tokea tuwe taifa na nina uhakika kabla hata ya kuwa taifa.

Lakini katika utawala uliopita tuliaminishwa mzunguko wa hela umebanwa na hivyo kupelekea kutokea upungufu wake mtaani/ mitaani.

Baada ya kumpata huyu Rais wetu mpya, aliye mpole na msikivu, mwenye kuongea Kiingereza kizuri kabisa 😉, tukaambiwa sasa mzunguko wa hela utarudi na hela zitakuwepo mtaani kama ilivyokuwa kabla ya kuja kwa dikteta Magufuli!

Sasa niaje raia? Mama kesharudisha hayo mahela mitaani?

Kama hayo mahela yamesharudi mitaani kwa nini mnalialia kuhusu vijitozo vya shilingi 100 mtumapo hela kwenye Em Pesa?

Kwa mnaojua hayo mahela yalipo, msiwe wachoyo. Tauambieni na sie wengine tuje tuyaokote bana.

Vilivyo vizuri kuleni na sie ndugu zenu.

Tuendelee kuupiga mwingi 😉.
Kwani zilienda wapi?
 
Ungekuwa wewe kwenye familia yako ungetaka kufanya jambo la maana ungekuwa umefanya kwa miezi minne au unajitoa ufahamu kwasababu unanafasi kulaumu?kama unataka kumfananisha mama na mwenda zake subiri miaka 6 aliyokaa.
 
Ajira bwerere? graduate atake mwenyewe kukosa ajira?
Wenzetu nyie mpo Tanzania hii hii au kuna nyingine?
Huwezi kulinganisha na kipindi cha kayafa jpm. Sasa hivi angalau huwezi kutembea na bahasha mara mbili au tatu ikakosa ajira. Wawekezaji wamemiminika sana hata manji anatafuta wafanyakazi sasa maana alifunga biashara zake zote na mo alitaka kukimbia nchi. Kila kona ilikuwa vilio hata ajira ndogo zilizokuwepo zilikuwa zinaueyuka daily kwa kuwakimbiza wawekezaji angalau mama kaja kurescu situation. Soon tutarudi kama enzi za kikwete ambaye alikuwa anajaniri walimu na madaktari wote bila kubakiza na wala bila kuaply unashtukia umepangiwa kituo.
 
Kwa sisi wapiga deal mambo yetu yanatunyookea taratibu...

Ngoja mama aendelee kuupiga mwingi kwa kutalii kwa majirani ili sisi tuendelee kuzichangisha...

Tumeanza kwa kujenga vituo vya mafuta kila baada ya kilometa 2.
Mwanza barabara ya buhongwa hakuna cha kulomita 1 ni mita 20 shell kila kilomita 20 shell mpaka najiuliza shell sa HV zinalipa sana?
 
Huu ujinga umesomea au umerithi? Serikali yenyewe imekiri imeweka tozo kwa kuwa hawana pesa na wakaenda mbali na kusema kama hatutaki tozo tuwaeleze pesa watazipata wapi.
Fanya kazi chawa ww sio kila inachosema serikali ukiamini, umesahau kwamba ni serikali yako hiyohiyo ilikwambia magu haumwi yupo ofisini anachapa kazi kumbe alishavuta kitambo tu,

Sema sina hela usizungumze jumla jumla
 
Kwa hiyo kama nchi maskini ndio hela zisiwepo mtaani? kwani kipindi cha JK nchi ilikuwa tajiri
 
Huwezi kulinganisha na kipindi cha kayafa jpm. Sasa hivi angalau huwezi kutembea na bahasha mara mbili au tatu ikakosa ajira. Wawekezaji wamemiminika sana hata manji anatafuta wafanyakazi sasa maana alifunga biashara zake zote na mo alitaka kukimbia nchi. Kila kona ilikuwa vilio hata ajira ndogo zilizokuwepo zilikuwa zinaueyuka daily kwa kuwakimbiza wawekezaji angalau mama kaja kurescu situation. Soon tutarudi kama enzi za kikwete ambaye alikuwa anajaniri walimu na madaktari wote bila kubakiza na wala bila kuaply unashtukia umepangiwa kituo.
Unemployment rate ya kipindi cha Magufuli na unemployment rate ya sasa kipindi cha Samia ikoje?
 
U
Naomba link tafadhali…
Usiwe mvivu wa kusoma ndo mana unapinga kitu ambacho hata hukijui. Nimeshakwambia NBS halafu unaniambia nikupe link, link gani sasa. Nyie ndo wale mnaosoma handouts badala ya kitabu kisa uvivu halafu unakuta ni wabisahi wakati hamjui chochote
 
Kwa magufuli unemployment rate ilikuwa 73% na kw samia ni 21% acvording to NBS(national bureau of statistics)
Mkuu unaelewa maana ya unemployment rate? Anyway, nakusaidia angalia takwimu hapa tokea mwaka 1991 then utapata majibu
Screenshot_20210802-211201_1.jpg
 
Hela itarudi mtaani baada ya utekelezaji wa bajeti ya mama kuanza,tathmni ni robo ya pili
 
U

Usiwe mvivu wa kusoma ndo mana unapinga kitu ambacho hata hukijui. Nimeshakwambia NBS halafu unaniambia nikupe link, link gani sasa. Nyie ndo wale mnaosoma handouts badala ya kitabu kisa uvivu halafu unakuta ni wabisahi wakati hamjui chochote
Mbona unakuwa mkali na unajihami? Wewe weka hiyo link hapa.

Mzushi mkubwa wewe 🤣
 
Back
Top Bottom