Hela zimesharudi mtaani?

Hela zimesharudi mtaani?

Nyani Ngabu​


Nilicho wahi kujifunza enzi hizo ni kwamba Dunia inaongozwa na makundi mawili yanayo jibadilisha kila wakati Wafanyabiashara na Wahalifu na makundi yote hubebwa au kuungwa (kwa hiyali au lazima) na kundi moja ambalo ni Wanasiasa. Ikitokea daraja (viongozi wa kisisasa) likashindwa au kuuamua kuyadhibiti haya makundi yatafanya kila hila kuhakikisha daraja linabomolewa na kujengwa walitakalo.

JPM was a bridge that decided to remain with ordinary citizens, to serve them by doing things that are worthwhile in the future and for all to benefited, that's when the cunning ones saw he wasn't on their side and the bridge had to be broken amekwenda Mzee wetu wa kuona matokeo chanya. Mapambio yakavuma ooh Mama ndio mleta faraja na kila sifa akapewa ...imekuwa kinyume waliosifia ndio wanao mponda. Na kweli maisha yanazidi kuwa magumu sana.... Corona ime take over kuliko kipindi chochote wakati ule kama nchi tuliuona mwelekeo ....sasa ndio tunakufa haswaa karibu kila familia imeguswa. Kodi za kijinga na zakikandamizaji zimetamalaki.

Mama anawachekea wafanyabiashara, nachofahamu hakuna mfanyabiashara au mwekezaji anayetaka kukipa kodi kwa hiyari wote lazima wabanwe ukiwachekea ndio hivyo expenditures unazikamua kwa ng'ombe mwenye njaa.

Chanjo hakuna asiye itaka ila imekuwa ni jinai, ujinga, ulimbukeni, ushamba na uzuzu kuhoji side effect zake, kisa kwa kuwa mzungu kaleta basi tukae kimya na kushukuru.... elimu kuhusu chanjo ilitakiwa itolewe, maswali ya madhara yajibiwe, sio kubeza na kuwaona wanahoji ni mambumbu.

Hela za kuokota zipo bandarini, kwenye miradi ya wakubwa na migodini ukiwa na kijinafasi cha maamuzi. Ila kama wewe ni wale tulioitwa na JPM wanyonge endelea kukamuliwa kwenye miamala.
 
watamkumbuka tu

1.wanaolalamika ubabe wa JPM ni wale walizibiwa mianya ya kula
unalazimisha tu, angalia namba moja hapo juu
Mjinga kabisa ule jamaa yeye aliziba vingine vya watu havizibwi
ushamba ulimtawala ndio maana alikuwa na tamaa mpaka kwa wake za watu.
Pesa za watu kazifuata mpaka Bank
upendeleo wa Ukabila na kukinyanyua Kijiji chake
safari tuna Rais ambaye hatakuwa na tamaa ya kukusanyia kwao mara uwanja wa ndege, mara Hosp, mara vyuo vya Veta yote ulimbukeni
 
Moja ya malalamiko ya kipumbavu kabisa yaliyokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli ni kuwa eti hela hazikuwepo mtaani.

Sijui ni lini hasa Tanzania hii ambapo hela zilikuwepo bwerere mtaani! Kwa sababu, Tanzania ni nchi maskini. Ni nchi ya ulimwengu wa tatu.

Vipato vya wananchi wake ni vya chini sana. Si nchi nyingi ambazo nchi yetu imezipita kwa vipato vya wananchi.

Na tumekuwa nchi ambayo wananchi wake ni wa kipato cha chini tokea tuwe taifa na nina uhakika kabla hata ya kuwa taifa.

Lakini katika utawala uliopita tuliaminishwa mzunguko wa hela umebanwa na hivyo kupelekea kutokea upungufu wake mtaani/ mitaani.

Baada ya kumpata huyu Rais wetu mpya, aliye mpole na msikivu, mwenye kuongea Kiingereza kizuri kabisa 😉, tukaambiwa sasa mzunguko wa hela utarudi na hela zitakuwepo mtaani kama ilivyokuwa kabla ya kuja kwa dikteta Magufuli!

Sasa niaje raia? Mama kesharudisha hayo mahela mitaani?

Kama hayo mahela yamesharudi mitaani kwa nini mnalialia kuhusu vijitozo vya shilingi 100 mtumapo hela kwenye Em Pesa?

Kwa mnaojua hayo mahela yalipo, msiwe wachoyo. Tauambieni na sie wengine tuje tuyaokote bana.

Vilivyo vizuri kuleni na sie ndugu zenu.

Tuendelee kuupiga mwingi 😉.
Mhuni kama mhuni
 
Uchumi huwa hauna urafiki.

Hata Rais atuchekee vipi swala la kuhakikisha kuwa uchumi unaimarika linabakia pale pale.
 
Back
Top Bottom