Yote uliyosema ni common sense tu mbona!
Unatumia kwanza anga. Baada ya hapo unaingia ardhini kulingana na malengo uliyojiwekea.
Vita vya kumtoa Saddam toka Kuwait vilianzia angani halafu baadaye ndo shughuli ya ardhini ikafuata.
Vivyo hivyo, vita dhidi ya Iraq ya 2003 ilianzia angani pia halafu baadaye ndo askari wa ardhini ndo wakaingia Iraq.
Au wewe unachotaka kuona ni askari wa IDF wakiingia Lebanon kichwa kichwa tu bila wana anga kufanya vitu vyao kwanza?
Huo utakuwa ni ujuha wa mwisho kabisa.
Hii siyo vita ya Banyamulenge na jeshi la Mobutu 🤣.
Vitani ni lazima uwe realistic. La sivyo mtafyekwa kama sisimizi.
Halafu, vitani ni lazima kutakuwa na casualties tu. Hilo haliepukiki na ni kwa pande zote.
Hakuna vita ambayo wanaokufa wanakuwa ni wa upande mmoja tu.
Hivyo, hata kama askari wa IDF watakufa, mwisho mshindi wa vita atakuwa ni IDF tu.
Hata Marekani walipoteza maelfu ya askari kwenye vita dhidi ya Iraq.
Lakini guess what? Walishinda vita.
Ni expectations za kijinga na kijuha kudhani kwamba baadhi ya majeshi askari wao hawawezi kufa vitani kisa tu eti wana superior military.
Lengo la vita huwa nalifananisha na boxing. Aim ya boxing ni to hit and not get hit.
Vivyo hivyo, vitani, lengo ni kuua na wewe kuepuka kuuliwa.
Lakini vilevile, inabidi uwe realistic. Kama ilivyo kwenye boxing, hata ukishinda kwa knockout, tuseme kwenye raundi ya 6, hiyo haina maana wewe hukupigwa ngumi hata moja na mpinzani wako.
Unaweza kushinda kwa knockout lakini nawe ukawa umetolewa nundu usoni.
Lengo la kutumia air superiority ni kurahisisha kazi ya jeshi la ardhini katika kupunguza risk.
Just simple, basic common sense ambayo hata mtu kama mimi nisiye na training yoyote ile katika military and warfare strategy, ninaiona ina make sense.