TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TatIzo hawa jamaa kila kitu wanaiga ukawa wenzenu hawana njaaa wananunua chopa mpya nyie kila sehemu mnataka piga deal angalieni sasa mnacheza na maisha yenu wenyewe kuweni waungwana jamani khaa

"Hawana Njaa Wananunua Chopa Mpya" Wangekuwa Hawana Njaa Wangepitisha Bakuli??
Unajua Maana Ya Kununua Chopa Mpya??
 
Mungu amlinde mwanamageuzi Deo Filikunjombe na baba Jerry silaha ambaye ni rubani

Mkuu Uhai wa hao watu uko mashakani sana. Cha muhimu ni kuwaombea tu Mungu awanusuru.
 

Attachments

  • 1444976062735.jpg
    1444976062735.jpg
    66.6 KB · Views: 658
  • 1444976077265.jpg
    1444976077265.jpg
    60.5 KB · Views: 728
hoops !kama no kweli badi ni janga la kitaifa jana sikuwahi kusikiliza taarifa ya saa tano itv ukweli zaidi ni upi?
 
"Hawana Njaa Wananunua Chopa Mpya" Wangekuwa Hawana Njaa Wangepitisha Bakuli??
Unajua Maana Ya Kununua Chopa Mpya??

Kwa iyo kupitisha bakuli ndo njaa? Acha ujinga wew jitu kubwa akili kisoda unafikiri kwa kutumia nin chadema chama cha watu huo ni utaratibu tu ambao upo hata wasipopitisha bakuli bado wananchi wataona hawajatendewa haki kwa kutochangia kwao, hivyoo ni lazima ujifunze kutofautisha kati ya ukawa na fisiem
 
Tony antony

Captain Silaa ni baba mzazi wa meya jerry Silaa ndiye aliyekuwa rubani ok
 
Last edited by a moderator:
Kwa iyo kupitisha bakuli ndo njaa? Acha ujinga wew jitu kubwa akili kisoda unafikiri kwa kutumia nin chadema chama cha watu huo ni utaratibu tu ambao upo hata wasipopitisha bakuli bado wananchi wataona hawajatendewa haki kwa kutochangia kwao, hivyoo ni lazima ujifunze kutofautisha kati ya ukawa na fisiem

Mkuu Wewe Uliomba Kuchangia Kabla Ya Wao Kutangaza Kupitisha Bakuli??
Huo Uchangiaji Miaka Yote Mlikuwa Wapi Kama Kweli Wanachama Mlikuwa Mnaona Hamtendewi Haki Msipochangia Chama Chenu?
Ccm Kadi Zetu Ndio Michango Yetu,tunazilipia....
 
Kutoka Clouds Deo hajapatikana hadi sasa na mawasiliank hakuna
 
"Hawana Njaa Wananunua Chopa Mpya" Wangekuwa Hawana Njaa Wangepitisha Bakuli??
Unajua Maana Ya Kununua Chopa Mpya??

Mkuu naamini umeongea hivi tu kwa sababu ya ushabiki ,kwani Chopa Mpya sh ngapi ???
 
Wanaukumbi.

Bado kikosi kazi cha idara ya wanyamapori kinamtafuta Deo Filikunjombe na wenzao waliopata ajali na chopa hapo jana.

Taarifa zinaeleza kuwa wametoka salama ktk chopa na waokoaji wameelekea huko alfajiri,mtoa taarifa wangu wakti anaondoka kanieleza kuwa huko hakuna mtandao.

Je tuombe timu ya uokoaji toka J'barg ama tuvumilie ndugu zetu watoke wenyewe toka kwa wanyama wakali.

Tunahitaji taarifa mpya toka selous.
 
Hata mimi nimesikia habari hizo....rubani nasikia ni Solomon Slaa ndugu yake Jerry Slaa.


Mungu apishe salama.....kwa waanga...

Lakini hvi ndani ya ccm....ukimuona mtu ni kiongoz au kijana au mtu mzima ni mpka kuwe na ukoo wote humo?? solomoni slaa dereva wa helcopter.....ya ccm kampen...huyu ni baba yake jerry slaa, diwani na meya wa ilala....!! hvi sisi baba zetu waliokuwa wanafanya viwanda vya zana za Kilimo UFI....tusubiri kufa kuingia ktk mfumo huu.....


ama kwweli kuondoa ccm ni muhimu ni kuondoa mfumo huu wa koo na familia katika kututawala.....shame,,,,,
 
Acheni uchochezi na kupotosha ukweli. Mwandosya hakusema amesusa bali alichosema ni kuwa anahamia kijijini kwao LUFILYO kwasababu amestaafu siasa. Kustaafu na kususa ni vitu mbali mbali ; muwe waangalifu na hayo mnayoandika!!

Hajasema ila Ukweli ni kwamba kasusia ndiyo maana amekuwa kimya kabisa
 
Mwenyekiti wa UWT Makambako anadai kuwa kuna sintofahamu kubwa kuhusiana na hatima ya mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa kwa tiketi ya CCM, ndugu Deo Filikunjombe, baada ya kuhusishwa na ajali ya helcopter iliyotokea usiku wa kuamkia leo.

Mwenyekiti huyo anakiri kuwa hadi leo saa kumi na moja alfajiri simu ya ndugu Deo haipatikani huku hata ndugu zake wa karibu wakiwa hawana jibu la uhakika kuhusiana na ndugu yao huyo.

Aidha sehemu ambayo ajali hiyo imetokea ni eneo lisiloweza kufikika kirahisi hivyo kishindikane kupata taarifa zozote za uhakika kuhusiana na jambo hilo.
 
Back
Top Bottom