TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Kama kuna Helkopta iliyoanguka basi siyo ya CCM. Uongozi wa chama umethibitisha uwepo wa chopa zote bila tatizo lolote

Nashukuru sana kwa taarifa hii na namwombwa MWENYEZI MUNGU IWE HIVYO yaani hakuna ajali hiyo regardless amebebwa nani.

Baadhi ya comment hapo juu zinadhihirisha kuna WATU na viatu hapa duniani! Yaana mtu unajitoa ufahamu na kumwombea kifo mwezio!!!
 
Mr Chin saa hizi upo Off? Maana kwenye hii ishu wewe pekee ndiye unaweza kutupa ukweli!
 
Last edited by a moderator:
Nna ugomvi na ccm but sio kwa Deo aisee..Mungu awaepushie hao manusura madhara zaidi.

Wewe hukai njombe mimi nimesomea njombe
Deo ni mbunge mnafki anayetengeneza picha na video aonekane mchapakazi
Ila kiukweli ni boya sana na ni mmoja kati ya wabunge wa ndiooooo!!tunahtaji wabunge kama kina lembeli ambao wanatengwa na ccm baada ya kuzungumza ukweli
 
Mungu aepushie mbali na wote wawe salama!japo ni mwana mabadiliko lakini naumizwa sana mwanadamu mwenzangu anapopatwa na maafa!wenzetu wanatakiwa washuhudie mabadiliko na walichoshindwa wao wenzao wakiweza huku wakiwa na afya tele!maana mwisho wa siku sote ni Watanzania na sote tuna nyama na damu!naomba hii taarifa iendelee kuwa tetesi na isiwe kweli!Mungu mkubwa!
 
Nimesikia tetesi somewhere kwa mtu nikasema ngoja nikimbilie huku, nako bado ni tetesi. Ila hii tetesi inaenda page ya tatu... Naomba Mungu isiwe hivyo, maana hata huyo mbunge kawa mentioned.
 
Siasa zisitufanye kuwa kama wanyama. Uhai wa binadam una thamani ya pekee sana hata kama ni audui yako au mna mitazamo tofauti. Yoh 3:16 inadhihirisha hilo, ewe mwanadamu u nani mpaka umuombee mwenzako kifo? Tuache hizi mambo jamani si nzuri. Huyo umuombeaye mabaya ana ndugu, watoto pengine wengine uko nao huko uliko. Utajisikiaje kama wewe mzazi, ndugu, rafiki ama jamaa yako wa karibu akiombewa ama kufikwa na hayo? Kuna maisha baada ya uchaguzi, tusijitoe akili. Sisi wote ni wa kupita tu.
 
Hilo tukio limetokea saa ngapi? Inamaana masaa yote haya pasipatikane taarifa kamili yenye uhakika na tunaishi na tetesi kwa tukio la ajali kama hii (kama ni kweli)?
 
Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous. Mungu aepushe kusiwe na majeruhi. Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye kampeni ziko salama.

#J. Makamba
 
Adui mwombee njaa tu. Sivema kushabikia kifo ila wkt mwingine huenda Mungu anamakusudi yake kuwaondoa hawa ma Ccm mmoja baada yamwingine ili watanzania tufike mahala tuishi kamatuko peponi kupitia rasilimali zetu.

Tunakuomba ewe mola wetu mtukufu uendelee kutuondolea kilamwenye nia mbaya nandoto zetu sisi waja wako, ndoto zakuishi salama ktk nchi yetu hii yenye kila aina yaneema ulizotujaalia.

Kila mpenda mabadiliko na aseme- Amen.

Kumbe huna akili hivyo dah we itakua yatima au teja nafkria hapa nashindwa nkuweke kundi dah mkuu we ujieshimu afu huna busara
 
Hizi habari ziko confirmed.moja ya ccm chopper imeanguka na kuungua moto majira ya saa moja usiku huko Selous.Waliofika hawajaona mtu wa kumwokoa,ilikuwa tayari usiku.Kuhusu nani na nani alikuwemo tusubiri asubuhi.Ila inasemekana ni Helicopter iliokodiwa na Deo kutoka Kenya.Ccm wana chopper kama 4 au 5 hivi.Tuvute subira hadi kukuche for latest.
 
Kama ni kweli mbona uchaguzi wa mwaka huu utakua ni kiyama kwa wanasiasa huenda matunguri wanayokwenda kufukiziwa na waganga wa kienyeji kwa kutumia viungo vya albino ili pate madaraka yameanza kuwatafuna wenyewe.
 
Back
Top Bottom