TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Ni kiongozi tulimuitaji katika kipindi hiki si kwa upande wa jimbo lake bali taifa kwa ujumla, alikuwa kiongozi hasiyejiona, aliyeishi maisha ya kitanzania, mchapa kazi, mwadirifu,mtu aliyeamini maendeleo ya jimbo lake ni watu kufanya kazi,aliwapenda watu wote bila kujali,vyama vyao vya siasa,alikuwa tayari kufanya kazi usiku mchana jua na mvua kuwaletea maendeleo wananchi wa tanzania,alichukia wizi na ufisadi na hakupenda makudi,

mungu haujatutendea haki kabisa katika kipindi ambacho taifa letu linaitaji viongozi wa namna hii kwa faida ya watanzania wote,
mungu akupumzishe mahali pema peponi

amina,

Unamlenga mungu yupi mkuu? maana naona umeandika kama unamwandikia JK!
 
Mungu Halaumiwi, Ni Kosa Kubwa Kusema Mungu Hajatutendea Haki, Wkt Wapo Watu Muhm Duniani Kuliko Filikunjombe Na Wamekufa.

Mshukuruni Mungu Kwa Kila Jambo.
 
Upepo mbaya CCM inatoka na watu. Tuweni makini na tumtangulize mungu katika maisha yetu ya sasa.

ntawashauri ndugu zangu wakiepuke,haiwezekani wanachama wake mashuhuri wanaondoka kwa kasi,yaani mpaka natetemeka, nahisi labda kiwaombe wachungaji wakiendeshee maombi mfululizo,kuna pepo lenye jicho moja NA mguu mmoja humo
 
Wanaukumbi.

Nyeti toka Lumumba zinathibitisha pasi na shaka kuwa January Makamba anataka kukwepa lawama.

Ccm imekodi chopa kadhaa na kukabidhi kwa makada waka akiwemo Filikunjombe (R.I.P) na alikabidhiwa kupambana na nguvu ya Lowassa Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Kwa nini alijihami toka jana kuwa iliyopata ajali haipo ktk mahesabu ya chama?

Je anakwepa kutuhumiwa kukodi chopa mbovu?

Aje hapa akanushe apewe ushahidi.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Wanaukumbi.

Nyeti toka Lumumba zinathibitisha pasi na shaka kuwa January Makamba anataka kukwepa lawama.

Ccm imekodi chopa kadhaa na kukabidhi kwa makada waka akiwemo Filikunjombe (R.I.P) na alikabidhiwa kupambana na nguvu ya Lowassa Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Kwa nini alijihami toka jana kuwa iliyopata ajali haipo ktk mahesabu ya chama?

Je anakwepa kutuhumiwa kukodi chopa mbovu?

Aje hapa akanushe apewe ushahidi.
Kwani capt. Silaa(R.I.P) ni mfanyakazi wa umma? Je amestaafu?
 
January anahusika vipi?
nani ni wataalam wa kutoa go ahead iwapo helicopter hiyo ni nzima na inafaa?
mamlaka husika zilishiriki?
 
Mkuu Inaweza Ikawa Lakini Mimi Sishangai Mkapa,nape,msukuma,bulembo Wanavoongea Wanavotaka Wamejipanga Kwa Huu Mchezo,na Ndo Mana Nahisi Wakina Mnyika Wamejiweka Pembeni,hii Mechi Bado Mbichi Hii #kikwete Vs #lowassa.......!!

Wewe jamaa ni mtu wa ajabu sana...Aisee yani mmmm...
Punde kidogo nimekusoma hapo nyuma ukisema kuwa Deo yuko ok, mara ukasema shughuli za uokoaji zinaendelea fresh tu ila shida ni kwamba watanzania hawasimami kwenye position zao! ndio maana hata magari ya zima moto yanakuwaga hayana maji kwa hiyo sio kosa la serikali, mara ukasema kikwete shida yake ni kwa vile ni mpole tu, mara ukasema wabunge wachaguliwe wa upinzani ila raisi awe magufuli...

Wewe jamaa ni mtu mwenye mambo vijiweni sana, ndo maana muda mwingi uko busy hapa kuwatoa watu nje ya mada, watu hapa wanatoa condolences wewe unaongelea ruzuku za chadema khaaa...sasa naona uko busy kushabikia na ku-boost ushirikina...dah!!!
 
Deo umekufa katika mapambano ulikuwa mzalendo wa kweli ; tutakukumbuka mno kaka; Mungu aitunze familia yake
 
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke,siku zake za kuishi si nyingi naye hujaa taabu,yeye huchanua km vile ua kisha hukatwa,hukimbia km kivuli wala hakai kamwe..(ayubu14:1-2) Ee Mungu tunakushukuru kwa maisha ya Deo hatuwezi kukuhoji kwa hili tunajua njia zetu si njia zako kadhalika mawazo yako si mawazo yetu ni km vile mbingu na ardhi zilivo mbali mbali,Amen.
 
Back
Top Bottom