TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Mwenyezi Mungu awaweke wanapostahili. Poleni familia na watu wote mlioguswa na msiba huu wa ndugu zetu.
 



makamba.jpg


Usiku wa kuamkia leo October 16 2015 headlines za siasa Tanzania zimetawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka na kulipuka kwenye mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).



Katika taarifa nyingine kutoka upande wa CCM iliyotolewa na naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba mida ya saa sita usiku ilisema >>> 'Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous. Mungu aepushe kusiwe na majeruhi. Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye kampeni ziko salama'


Baadae aliandika >>> 'Kwakuwa ilisemekana kuwa chopa ya kampeni ya CCM imeanguka, tulifuatilia/kubaini/kuripoti kuwa tulizokodi kama Chama hakuna iliyoanguka' hiyo ndio ilikua tweet ya mwisho kuandika na January Makamba usiku huo lakini badae aliRT kilichoandikwa na Waziri Nyalandu na Zitto Kabwe.



ZITTO through FB >>>>
Ndugu yetu, rafiki yetu na mzalendo mwenzetu DeoFilikunjombe ametutoka kufuatia ajali ya helkopta.Nawasihi tuwe na utulivu wakati huu mgumu

ZITTO through FB >>>> Naomba utulivu.1)ajali ya helkopta imethibitishwa 2)kuwaka hakujathibitishwa 3)ndugu yangu Deo alikuwamo 4)hakuna uthibitisho wa madhara...


kandiliyetu.com
 
Kuna habari kuwa chopa lililokita chini huko selous ilikuwa imebeba fedha kiasi cha 10b hizi ilikuwa nikwaajili ya kwenda kuuwa upinzani nyanda za juu kusini,
 
Kazi ya mungu haina makosa umeodoka mpendwa wetu bado tunakuhitaji kushinda kipindi chochote lakin mungu kakupenda zaid (Mzalendo wa kweli mpenda nchi umenitoa machozi )

Mkuu hii sio kazi ya MUNGU niyawanadamu MUNGU hajanunua madege mabovu
 
Mkuu zile zilikuwa habar tata sana, kwanza ndege iliangukia katkat ya mbuga, hivyo hakuna aliyekuwa na uhakika kwasababu hapakuwa na msaada wowote mpaka ilipofika jana saa8 kasoro za mchana.

Kwanza ilikuwa bahati tu mzungu mmoja mtalii ndiye aliiona helkopta ikipita na baadae akaona mlipuko mkubwa ndio akasaidi kutoa direction ya eneo hilo lakn hata hvyo haikuwa rahisi kufika lile eneo kwa gari isipokuwa kwa chopa tu.

Ndio maana mpaka jana mchana hakuna aliyekuwa na taarifa za uhakika juu ya uwepo wa majeruhi au vifo.
 
Huyo anaesema chopa zao zilikuwa salama.......alitoa wapi hiyo taarifa......?.....au Bumbuli.....?......hawana mawasiliano ndani ya chama chao.....?......
Iweje muwe na ndege msijue ipi ipo hewani.......na ipi hairuki.....?......
Kweli CCM wanazidi kujimaliza wenyewe kwa uongo bila kujua........
 
Mambo ya kujiliwaza tu! Nasubili nione hizo nne zilizobaki, nani atazipanda na kuweka manjonjo ya kuiga.

Hii ni nchi isiyo na viwango. Tumecheza na viongozi chini ya viwango, hospitali chini ya viwango, barabara chini ya viwango na sasa nikiambiwa chopa zote zilizoletwa ni chini ya viwango, sitaona ajabu. Mambo yote tunawaza dili tuuuuu!

Ndio maana hata NDEGE ya Serikali naiogopa sana kupanda cz wanaonunua wanajali cha juu tu....Likiporomoka huko hakuna anaejali...2sad
 
Mkuu@ Zungu Pule DEO kwenye lile jimbo alikuwa anasubiri kuapishw tu so hata km angetumia Baiskeli kufanya Kampeni angechaguliwa so hakuwa nasababu yakukodisha CHOPA taarifa zilizopo nikwamba CCM baada yakujua jamaa anakubalika na jimboni kwake hakuwa na kz kubwa waliamua kumkodishia chopa akatie KAMBI kwenye mikoa ya Nyanda za Juu kusini maana huko ukiacha MWANDOSYA hakuna mwingine anaekubalika kwa sasa na Mwandosya hamkubali mgombea wa sasa....Tafakari
 
Wasemaji wa ccm wamebadilika?Naona kama Nafasi ya Nape imeshikiliwa na Kina Makamba et al.
Kila moja anakua na taarifa zake bila wao kuwasiliana.
R.I.P FILIKU
 
Waacheni waliolala mauti walale kwa Amani. Watanzania tunapita ktk kipindi kigumu sn matukio ya ajali ni mengi na kila saa tunahoji utadhani tunamfundisha mungu kufanya kazi yake. Na serikali ikifanya kila inaloweza kuficha baadhi ya mambo.tuombe mungu tuvuke kipindi hiki salama.
 
Nilipoona kwenye ukurasa wake wa fesibuku nikajua tu ataumbuka,

Maana ajali itokee jioni teka katikat ya mbuga za wanyama, yey anakurupuka kutetea usalawa wa chombo badala ya kutafuta ukweli, kweli hawa watu hawa,,........

Kukurupuka tu.......ilikuwa rahisi sana.......angepiga simu tower ya ilipoondokea......then aulize.........wangemwambia.......akiwa kama waziri wa mawasiliano.......alitakiwa achukue hatua hiyo mwanzo........
sasa mtu unakurupuka kutokea from nowhere........unakana kuwa ndege zetu zote zipo salama........au ilikuwa ni dhambi kwa hiyo chopa kuruka.......?.......kukana kwao inawezekana ndiko kulikosababisha wapendwa wetu kukosa msaada mapema........&$€#¥o kabisa.....
watu wengine wanaboa sana........
 
Makamba Jr sikujua kama wakati mwingine huwa mpumbavu, nyumbu kuzidi hata wale wanaowaita malofa! Yaani hiyo kambi kila mmoja anafanya kivyake hakuna mawasiliano, kila mmoja anamwona mwenzake kama anajipendekeza kwa Magufuli. Kazi wanayo kwa kweli, lazima mwaka huu tuwakalie nyoko hawa!! Ingekuwa nchi za wenzetu kauli hiyo tu ilikuwa inatosha kumfanya ajiuzulu nyadhifa zake ndani ya chama!!
 
Back
Top Bottom