Kuna haja kubwa sana ya kuanzisha forum ya "MAKING MONEY ONLINE".
Wabongo ilibidi tuwe mbali sana hizi vitu kwasababu internet ni bei rahisi sana na speed ni nzuri ila inatumika kuchekia udaku insta, kufowadi memes / vichekesho groups za WhatsApp, kuangalia porn, na takataka kibao, huko south Africa 1 GB inabidi ujipinde ulipe kama msimba hivi.
Kuna fursa nyingi sana online hata kama huwezi chochote unaweza kununua Huduma kwa bei rahisi na kuuza kwa Wateja wa marekani kwa bei ya juu, kwa mfano unaweza kwenda huko fiverr ama up work ukajinadi wewe ni mchoraji kumbe hujui, ukipokea kazi unaenda kwa vibanda vya wachoraji wakare wanakuchorea hata kwa buku 5 michoro iliyonyooka wewe unauza kwa dola 5 na kadri unavyozidi kusifiwa unatoza 10 unaenda mpaka 20.
Kuna lundo la waburudishaji huko insta ambao huenda hawaingizi chochote ila wanatoa burudani kwa followers wao bure kabisa labda wakibahatika kupost matangazo ya dawa za nguvu za kiume ndio wanapataga hata teni, aina hii ya watu ilibidi wawe na blogs ama apps zao zilizo na ad networks kama AdSense, propeller ads, adsterea, medianet. N.k, wanaposti stories au video nusu then wanashawishi followers wakatazame video nzima kwenye blogs ama apps zao ili wafaidike kwa kuingiza pesa.
Katika dunia ya Leo ukijiongeza huwezi ukatamani ajira hizi za maofisini za laki 5, ajira za online zinalipa mno hasa ukiangalia sisi hapa kwetu matumizi ni madogo, unakuta unaingiza hata dola 100 (220,000 pesa ya madafu) kwa siku ambayo kwa nchi za ulaya zinazolipa mshahara wa chini elf 20 kwa saa ni hela ya kawaida ila kibongo bongo hapa ushawini .
Changamoto inapokuja ni kwamba wabongo wengi wanaofanya hizi online works (ukiachana na forex) ni wachoyo wa ramani na kuna baadhi yao wanadanganya kuwa wanaingiza pesa mtandaoni ili wapate wanafunzi wataolipia ada ya darasa kumbe wao kama wao hawajawai kuingiza hela katika kile wanachofunidisha, ukitaka kuwajua ulizia ushahidi wa hela waliyoingiza na miamala ya kutoa hizo pesa, wengi huishia kubwabwaja maneno.