Heri tukose misaada kuliko kuamrishwa nini cha kufanya na Ulaya

Heri tukose misaada kuliko kuamrishwa nini cha kufanya na Ulaya

Uhuru wetu utakuwa mashakani kama tutaendelea kutegemea misaada kutoka nchi za Magharibi. Mama yule anayemlipa mwimbaji ndiye atakaechagua wimbo.

Ndugu zangu tuwakumbushe viongozi wakusanye Kodi kwa Kila mtu na kila kazi Ili tupunguze kutegemea misaada. Na sisi raia tuwe wakali vya wanaotuibia Kodi zetu.
Soma pia kuhusu neocolonialism na kwanini tunatumia teckonolojia zao na kila wakisasisha hizo tekinolojia, (technology), tunaenda tena kusoma

Kwakifupi viongozi wa kiafrika ni wabinafsi halafu ni wapumbavu, mpumbavu ni mtu aliyebobea kwenye taaluma fulani ama jambo fulani lakini halifanyi kwa weledi majukumu anayo pewa kwa Tanzania upumbavu ni kipaji
 
Hamshindwi kujitegemea bali ndio mmeufanya mfumo wenu wa maisha.

Mnajiona walemavu msioweza kujitegemea kwa lolote.

Ukianza kuwa ombaomba basi usitegemee kuacha kwa sababu serikali ndio imeufanya uwe mfumo wa maisha.
 
Ukiweza kujitegemea ndio unakuwa na maamuzi/kauli. Bajeti yenyewe asilimia 60/70 ni misaada kutoka kwa mabepari, achana na hizo chanjo na misaada miingine wakichomoa nyaya utaweza kufunga mkanda? Boss hanuniwi mbwa wewe
Kama Kuna kiongozi anaedhani haiwezekani bila misaada yao atupishe. Sisi tunafahamu Magharibi wana watu wao huku, maana kunguru hana kibyongo. Tuachane na Kila aina ya misaada anayotweza Uhuru wetu wa kujiamulia. Tunaweza kuhamia uchina na Afrika humuhumu. Na ukishajua huna mjomba utaacha kudeka.
 
Ukiweza kujitegemea ndio unakuwa na maamuzi/kauli. Bajeti yenyewe asilimia 60/70 ni misaada kutoka kwa mabepari, achana na hizo chanjo na misaada miingine wakichomoa nyaya utaweza kufunga mkanda? Boss hanuniwi mbwa wewe
Viongozi wetu hawakusanyi kodi ipasavyo. Watu wachache sana wanalipa Kodi. Kwenye bodaboda tu unaweza kupata pesa ya kununua madawati nchi nzima, kwa machinga tu unaweza kupata pesa ya kununua dawa hospital zote za umma.
 
Waya wa umeme umeenda mbali sana. Ardhi ipo mambonde ya kulima miwa yapo. Kuna ardhi kwaajili ya kilimo cha mahindi na mpunga. Ipo misitu ya kutosha binafsi na ya serikali Kama ule wa mafinga.
Vipi upatikanaji wa Sukari
Mchele je?
Tooth picks tunajivunia toka china
Karatasi je
Ndio tuseme hatuitaki msaada toka kwa mtu anaetuelekeza kuwa tusiumizane?
Kwahiyo unataka serikali itengeneze toothpicks? Hata huko China sio serikali inayotengeneza toothpicks, kwanini wewe usitengeneze na kutuuzia, badala yake miti ya kutengeneza toothpicks unachoma mkaa.
 
Unatutakia nini wewe, eti tuwe wakali kwa wala kodi zetu, hao wala kodi zetu unadhani wanataka hata kuambiwa kitu, achilia mbali kusikia, mwishowe watukamate kwa kuwaambia ukweli wakatitoe roho zetu
 
Yaani wewe shida yako tu umkamate Lissu baasi na umuue Kitima?
Ulaya watusaidie kwanza kutatua shida wacongo, DRC, Sudan, Somalia, Ethiopia, Ukraine, Palestine, Sahel na Libya kabla ya kutaka kutatua shida za watanzania. Tutawashukuru sana.

Akina Ndugai waliona mbali kuhusu kutegemea misaada n mikopo kutoka kwa wakoloni wetu. Tunafahamu wakoloni wana watu wao humuhumu miongoni mwetu, ushahidi wa wasiwasi wetu ndio huu.
 
Uhuru wetu utakuwa mashakani kama tutaendelea kutegemea misaada kutoka nchi za Magharibi. Mama yule anayemlipa mwimbaji ndiye atakaechagua wimbo.

Ndugu zangu tuwakumbushe viongozi wakusanye Kodi kwa Kila mtu na kila kazi Ili tupunguze kutegemea misaada. Na sisi raia tuwe wakali vya wanaotuibia Kodi zetu.
Uhuru wa kutekana na kupotezana sio? Au uhuru wa kubambikia watu kesi?

Kama hatukua tayari kwa mfumo wa vyama vingi, warudishe chama kimoja ieleweke. Kuliko haya machungu mnayowajazia watu mioyoni. Mwisho huwa mbaya
 
Uhuru wa kuwaneemesha wachache na kukandamiza walio wengi 🚮🚮
 
Viongozi wetu hawakusanyi kodi ipasavyo. Watu wachache sana wanalipa Kodi. Kwenye bodaboda tu unaweza kupata pesa ya kununua madawati nchi nzima, kwa machinga tu unaweza kupata pesa ya kununua dawa hospital zote za umma.
Shida sio walipa kodi. Shida inaanzia kwa wakusanya hizo kodi. Wanazifanyia nini? Au wanajigawia kwa urefu wa kamba zao?

Tungeanza na katiba yenye kumnyang'anya mamlaka rais.

Wakina lissu wanapigania no reform no election ndo ulikua wakati wa kuwaunga mkono ili tufike unakotaka
 
Back
Top Bottom