Heri Udikteta Kuliko Maigizo ya Demokrasia

Bora maigizo maana walau yanakupa nafasi ya kupumua kidogo kuliko kufugwa kama Nguruwe.

Kama udikteta ni mzuri hamia Rwanda na kwingineko

Unataka uishi katika ukweli ili uwe free or katika uwongo ili uzidi kuapat false hopes na kumaliza energy katika vitu ambavyo havipo?
 
Kawadanganye wanao
 
Kawadanganye wanao
Kwa nini niwadanganye? Nawaeleza kilichopo.Umewahi sikia Watanzania wanakimbia Nchi Yao kama hao mnaowasikia wanafia kwenye malori na baharini Mediterania?

Tena Serikali iendelee kupiga Pini Machadema hivi hivi wasituletee blaa blaa zisizo na msingi.
 
System ipi hauingizwi kama Ng'ombe? Wewe ndio huna dira au hujui kama Tanzania inatekeleza dira ya 2025 na Sasa dira ya 2050 inaandaliwa.

Ujinga wako usitujumuishe wote.
Dira unaelewa maana yake? Au ndo utekeleezaji wake ndo huu wa kujenga majengo yasio n walimu? Maabara zilizokosa ata vernier caliper? Au dira gani unazungumza mzee. Unatetea ata ambacho ukielewi na unaowatetea awaelewi
 
Unataka uishi katika ukweli ili uwe free or katika uwongo ili uzidi kuapat false hopes na kumaliza energy katika vitu ambavyo havipo?
Ukweli upi na uongo gani? Partial democracy is real ni sawa na mixed economy Sasa hapo Kuna shida gani unaiona?
 
"Mtanikumbuka kwa mazuri, si mabaya" JPM
 
una shida mahali, kutokimbia nchi sio kuridhika mitanzania mingi mijinga bora ife na njaa kuliko kuonesha awaridhiki
 
Dira unaelewa maana yake? Au ndo utekeleezaji wake ndo huu wa kujenga majengo yasio n walimu? Maabara zilizokosa ata vernier caliper? Au dira gani unazungumza mzee. Unatetea ata ambacho ukielewi na unaowatetea awaelewi
Ona Sasa unavyokurupuka na kuruka ruka.Dira ya Maendeleo ya Tanzania inayoishia 2025 ilisukwa 2005.Hicho unachoita Madarasa yasiyo na walimu ni sehemu ya kuteleza dira kwenye sekta ya Elimu.

Kwani wewe unadhani dira Huwa inatekelezwaje?
 
Wee kiaziii kwaheri
 
una shida mahali, kutokimbia nchi sio kuridhika mitanzania mingi mijinga bora ife na njaa kuliko kuonesha awaridhiki
Usilazimishe shida zako kuwa za Watanzania.Mnavyojifanya mna akili ndio kwaanza wanazidi kuwapuuza.

Watanzania wangekuwa hawaelezei kutoridhika kwao Serikali ingetulia tuko bila kufanya kitu.

Kama huridhiki sio kazi ya Serikali kuridhisha mtu binafsi,hiyo kazi anaiweza mkeo , Serikali inafanya jambo la manufaa Kwa jamii ya walio wengi.

Mwisho wewe huridhiki na kipi Sasa kutoka Kwa.Serikali?
 
Waulize walimu ,nenda kaishi kigogo mburahati manzese buguruni mbagala na waulize kama wanaridhika na serikali yao, nenda uko bukoba vijijini nenda uko songwe vijijini ukaone watu wanavoishi labda utapata akili
 
Lakini Maza hana nia ya dhati kurudisha Demokrasia iliyokuwepo kabla ya Magufuli.
Acha mzaha wewe,kabla ya Magufuli kulikuwa na Demokrasia gani ambayo saizi haifanyiki? Yaani kipi kilifanyika awamu ya JK ambacho saizi hakifanyiki?

Waswahili wana Msemo kwamba Bora umfadhili mbuzi utakunywa mchuzi sio binadamu.Ni Samia huyu huyu ndio kawapa nafasi watoe Mapendekezo Ili sheria ya uchaguzi inadilishe hii hii ambayo ilokuwepo enzi ya JK.
 
Wanaotaka hayo wawahi Rwanda,Niger,Burkinafaso watapumua tuu na kufugwa kama Nguruwe
Sasa kwani Watanzania wana tofauti gani na hao uliowataja?Nitajie nchi ya Kidemokrasia ambayo watu wake wanaishi maisha ya kilofa kama Tanzania!
Ni bora Bi.Mchele awe muwazi kama Jiwe,yeye alijipambanua wazi kuwa hapendi kupingwa na ndiyo maana hatukuona kamati na vikosi kazi vya kisanii vya kuimarisha Demokrasia ambayo haipo.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Waulize walimu ,nenda kaishi kigogo mburahati manzese buguruni mbagala na waulize kama wanaridhika na serikali yao, nenda uko bukoba vijijini nenda uko songwe vijijini ukaone watu wanavoishi labda utapata akili
Bahati mbaya hakuna Serikali ya kukutafutia maisha.Hao walimu mnaowataja Wana maisha mazuri kuliko Watumishi wengi wa Halmashauri na Wizarani.

Na Mimi nasema waulize wakulima wanataka warudi Misri au safari iendelee? Waulize Wafanyabiashara wanataka warsudi Misri au safari iendelee? Na mwisho Uliza Watumishi Kwa ujumla wanataka warudi Kwa Sera za Mwendazake au tusonge mbele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…