Herufi R na L ni tatizo kwa Rais wetu, tumsaidie

Wazalamo=Wazaramo
Mtakosoa Sana , lkin hizo ni minor case Sana coz hata watz wengi nikiwemo Mimi wazalamo huwa wananikosoa maneno mengi na huwa wananicheka
 
..asante.

..nimejifunza kuwa tunapaswa kuandika, " vita vya pili vya dunia. "
Sawa Mkuu,.. "Nani kaanzisha vita vya pili Vya dunia" sio "Nani kaanzisha vita YA pili ya dunia"..

"Miaka MiNANE ya maendeleo" sio "Miaka NANE ya maendeleo"..

Hayo ndio baadhi ya makosa sugu ya waandishi wa kiswahili wa humu JF, na baadhi ya Watanganyika..
 
Utatekwa mkuu
 
kiswahili wanadai kilitokea congo huko kwahiyo kilichelewa sana kufika chato
 
Sasa naona mnataka mkuu wa nchi abadilishe lugha ya taifa iwe kisukuma.
 
Lugha yetu ya taifa ambayo tunaifanyia bidii kuisambaza Afrika na nje ya Afrika sisi wenyewe ndiyo tumekuwa wa kwanza kuiharibu.

Tukitaka kukienzi na kukilinda Kiswahili fasaha basi somo la Kiswahili mashuleni liambatane na kufundisha irabu za asili zilizokuwa zikitumika kwa mamia ya miaka kuandika Kiswahili. Si nyingine ni irabu za Kiarabu.

Waliosoma irabu za Kiarabu iwe usukumani au popote pale, wanakuwa hawana shida ya kuzitamka au kuzichanganya R na L.

Mlinda asili ni jasiri.
 
Labda ni kweli sio mtz. Maana warundi, waganda, wanyarwanda wakija tz kiswazi huwapa dhida na hudhindwa kutifautsha R na L katika matamdhi.
 
Sio rais tu kwani hata humu jf hulioni?
 
"Ng'wabheja na sio mwabeja"
 
Watu wengi wa kanda ya ziwa hizi herufi mbili wanazichanganya sana mkuu....inaweza kuwa wanaathiriwa na lugha mama
 
Huwezi kupingana na nature na wala huo sio ujinga au kutokujua. Ni asili yake wote wako hivyo mkuu. Ni kawaida sana ilimradi unamuelewa muache tafadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…