Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ndivyo watawala wa chama tawala wanavyoendesha nchi hii. Makosa yanayofanywa na watu wao huwa kila jitihada itafanywa kuyafunika. Na hawaoni aibu juu ya hili, huwa wanasema waziwazi ukiwa mtu wao watakulinda. Kwa maneno mengine kuwa mtu wao kunakufanya uwe juu ya sheria.
Na kibaya zaidi, Polisi wanajua hilo, kwamba wakitaka kazi zao ziwe salama, basi waelewe kwamba watu wa chama tawala wako juu ya sheria. Hata wakiua, wakibaka, wakisafirisha wageni haramu, wakikutwa na madawa ya kulevya au nyara za serikali, wakifanya maandamano bila kibali, wakifanya lolote lile, hawapaswi kubugudhiwa.
Na Polisi wameambiwa tukio la kihalifu linapofanywa na mtu wa chama tawala basi watalitolea maelezo ambayo hayatakichafua chama tawala, hata kama inabidi waseme uongo. Kifo cha risasi au kupigwa kitabadilika kuwa kifo cha shinikizo la damu, nk.
Ndio maana basi, japo maneno makali kuhusu mmiliki wa jengo la Kariakoo yaliyotolewa na waziri mkuu, polisi walipowaambia watawala mmiliki wa jengo ni mmoja wenu katika chama, waliamriwa wakae kimya hadi uchaguzi wa serikali za mitaa upite. Jitihada hata zilifanyika kujaribu kubadilisha jina la mmiliki, na huenda zimefanikiwa tayari.
Hii ndio Tanzania yetu. Au Tanzania yao?