Hesabu ya dereva wa daladala Baada ya nauli kupanda

Hesabu ya dereva wa daladala Baada ya nauli kupanda

Naomba kujua kama hesabu ya siku ya dereva wa daladala has Dar, inatakiwa ipande kwa kiasi gani ?

Kwa sababu vipuri vimepanda bei sana .

Nina daladala 3 zinatoka buza hadi mnazi mmoja na kwa siku nakusanya 75000 kwa kila daladala, Niongeze kiasi gani kwa haya mabadiriko ya nauli yalitangazwa .
75000 baada ya kutoa gharama zote?
 
UKWELI zama kwenye daladala mwenyewe....tembea humo kwa siku kadhaa ndio utapata uhalisia.....mengine ni porojo za mezani na hesabu ya calculator...nimeshuhudia makampuni yaliyofanikiwa maboss huingia front kwenye uwanja wa mapambano then wanashiriki na madereva kutatua changamoto Ref. Omar Bakhresa....anatembea na lori kuona changamoto(trust me).
 
Hiv wale wamiliki wa mabasi mfano basi la kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza wanafunga hesabu kwa shilingi ngapi, yaani hela ya boss ni ngapi? Nauli ni 70,000
 
Naomba kujua kama hesabu ya siku ya dereva wa daladala has Dar, inatakiwa ipande kwa kiasi gani ?

Kwa sababu vipuri vimepanda bei sana .

Nina daladala 3 zinatoka buza hadi mnazi mmoja na kwa siku nakusanya 75000 kwa kila daladala, Niongeze kiasi gani kwa haya mabadiriko ya nauli yalitangazwa .
Usi copy na ku paste kaa chini piga hesabu mwenyewe, usidhani hesabu zinafanana, ukiwaiga watu humu unaweza kuyumba kibiashara
 
Asante kwakumeguamegua hii hesabu maana wengine ni slow learner
Faida haiwezi kuongezeka nyingi hivyo
Hiyo hesabu inakosa ongezeko la bei ya mafuta, hivyo itakuwa sahihi tu kama anayeweka mafuta ni Boss (mwenye gari); ila kama anayeweka mafuta ni Konda/dereva huo mchanganuo sio sahihi
Hapo kwenye % unatakiwa utoe 10% fuel inflation; inayobaki ndio uongeze kama makusanyo/faida
 
Naomba kujua kama hesabu ya siku ya dereva wa daladala has Dar, inatakiwa ipande kwa kiasi gani ?

Kwa sababu vipuri vimepanda bei sana .

Nina daladala 3 zinatoka buza hadi mnazi mmoja na kwa siku nakusanya 75000 kwa kila daladala, Niongeze kiasi gani kwa haya mabadiriko ya nauli yalitangazwa .
nauli imepanda kutoka sh 100 mpaka 150.
piga hesabu ujue hii ni asilimia ngapi ya kupanda kwa nauli.

ambayo mfano piga

550 = 100%
700 = ?

utakuta roughly nauli imepanda kwa asilimia 1.3 (nimeongeza kidogo digits)
Screenshot_20231130-131545.jpg

sasa ndugu yangu na wewe chukua 1.3 zidisha kwa 75,000 utapata kiasi chako unachopaswa kuletewa kila siku..

ambacho ni
Screenshot_20231130-131724.jpg

na uwaelimishe watu wako kabla hujawapa mkeka mpya...

mwisho kabisa boss naomba elfu 10 sina nauli naelekea katoro kufanya interview...
 
Back
Top Bottom