Heshima kwa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema

Unamaanisha Tundu saivi rally aliyonayo inawiyana na Ile ya Mrema?
Ulikuwa hujazaliwa. Mrema alikuwa tishio zaidi ya Lowassa. Hadi leo haelewi kwanini hakushinda.
Nakumbuka siku aliyojiondoa CCM akiwa waziri, alibebwa juu juu na akapewa Nissan patrol na mfanya biashara mchaga mwenzake pale dodoma.
Yule jamaa baada ya uchaguzi na mrema kushindwa alipelekewa Kodi na mamlaka ya mapato ya tsh 200 mil, mwishoni jamaa alirudi CCM.
 
Usilinganishe Watanzania wa mwaka 1995 na wa 2020 huo ni upoyoyo
 


Hata Malawi walisema ni mbwembwe mwisho wa siku wakabaki vinywa wazi
 
Anachokisema mtoa mada kwa maana nyingine ni kwamba CCM na NEC yao ni wabobezi kwenye kuchakata kura na wameanza toka 1995.

Ni kweli kwamba mambo mengi yamebadirika sana since 1995 lakini ambacho hakijabadirika ni hii NEC. Nadhani CCM wao wala hata hawatishiki na nyomi kwenye mikutano ya Lissu maana wanajua game huwa linamalizwa wapi
 
Mrema, lowasa pia kumbuka nguvu kubwa ya ukaskazini ilitumika kwa kuwasapoti huyu Lisu hilo halipo wala ukati hawamsaport ataambulia 3% ya kura zote zitakazo pigwa
 
Kiutani utani hivi hivi...

Bandu bandu Lissu humaliza gogo!

Malawi ilikua hivi hivi,see what happened?

Sio kila siku ziko sawa ndugu
 
Mrema, lowasa pia kumbuka nguvu kubwa ya ukaskazini ilitumika kwa kuwasapoti huyu Lisu hilo halipo wala ukati hawamsaport ataambulia 3% ya kura zote zitakazo pigwa
if is that so,mbona mnapaniki namna hii?

naona unagawa percent kwa wagombea,ushamgea Lissu 3%,sijui wewe ni nani unagawa hizi percentages?

Malawi walikua wanasema hiv hiv,matokeo ya kura yalipotoka,walishangaa...

Sio siku zote ni sawa
 
That was 1995 this is 2020 almost 25 years back, mambo yamebadilika sana kuanzia teknoloji, uelewa, tabia za watu na hata vijana wengi wanaopiga kura leo walikuwa hawajazaliwa, Mzee Mwinyi alisema kila zama na kitabu chake.
 
Katika kusoma na kujifunza Mambo Historia huandikwa na waliopo kwa ajili ya vizazi vijavyo, kwasababu sasa wote wawili Mrema na Marando ni watu wazima tuseme sasa ni Wazee, ni vyema waandishi wa habari wangejitokeza na kuwahoji nini kilitokea kati yao, na Mrema aseme kama kweli alihujumiwa na alihujimiwa vipi, Marando aseme chanzo cha gogoro lile ni nini na Msajili Tendwa nae aseme kwa ajili ya kuandika Historia na kutambua michango yao.

Kwa hakika watu hawa wakiamua kuandika kitabu kitakua cha kusisimua sana kabisa.

Bahati mbaya wandishi tulionao leo hii sio wengi wabunifu na wachache wabunifu akina Paskali sijui kama wataamua kuchukua hili wazo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…