Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefafanua kuwa inatoa mkopo kwa Wanafunzi kulingana na siku za masomo kwa kila robo ya mwaka wa masomo
Imeeleza kuwa kutokana na COVID19 siku za masomo za robo mwaka ya nne ya muhula wa masomo wa 2019/20 ambazo huwa ni 60 zimepungua kwa baadhi ya Vyuo ambapo baadhi vyuo vimebakiwa na siku 45 za masomo
Imesisitiza kuwa Wanafunzi watakaosaini wataona kwenye nyaraka zao kuwa fedha zimepungua kulingana na siku za masomo watakazokuwa nazo kuanzia Agosti 01
Aidha, Bodi imeongeza kuwa kuhusu kuwaarifu Wanafunzi juu ya suala hilo, wao wanaongea na Chuo kwa maana taarifa za Wanafunzi wanaosoma ikiwemo matokeo wanapewa na Chuo husika
Pia, mabadiliko yote ya Chuoni ikiwemo siku za masomo na mikopo, yanajadiliwa kwenye Baraza la Chuo ambapo Viongozi wa Wanafunzi wapo, hivyo kama wanafunzi hawana taarifa hizo wanatakiwa kuwauliza Viongozi wao
Kuhusu ada kulipwa yote bila kukatwa, Bodi imeeleza kuwa siku za masomo zimepungua ila muda wa masomo kwa siku umeongezeka na kufanya walimu kuendelea kufundisha kwa muda ule ule kama ambavyo siku zingekuwa hazijapungua
Baadhi ya Wanafunzi katika Vyuo mbalimbali walilalamika kukatwa fedha za mikopo (Boom) bila kupewa taarifa japokuwa wao waliingia mkataba na HESLB na pia walidai wamekatwa ‘Boom’ ila ada haijakatwa
Pia, soma HESLB: Serikali imeanza kulipa Malipo ya robo ya nne ya Mwaka wa Masomo 2019/2020 kwa Wanafunzi 132,119 Jumla ya TZS 66.9 Bilioni