HESLB: Hatujapunguza mikopo ya Wanafunzi. Tunatoa fedha za kujikimu kulingana na siku za masomo

hapo sio sawa
 
vilevile hiki ni kipindi Cha Corona wanafunzi wameongeza matumizizi mengine Kama vile barakoa na sanitizer, na usafiri umepanda Bei hasa kwa wanafunzi wanaosomea dar coz of level sit, na zaidi tulitarajia kuona hela ya kujikimu inaongezwa kusudi wanafunzi waweze kujikinga na Janga korona, kitu kingine bodi haijazingatia hali halisi ya wanachuo kwani kipindi Cha likizo nyumba wanazoishi wanachuo hazikusitisha Kodi Bali iliendelea, na Kama ingekua hvi Basi tungeambiwa tokea vyuo vnafungua ili watu wajipange kisaikolojiaa juu ya kulikimu hili suala,
 
Pesa ya chakula inalipwa kwa siku
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu umeanza vizuri kabisa kwa kueleza kwa hoja Ila hapo mwisho umekuja kuharibu kabisa baada ya kuleta Mambo yenu ya vyama na siasa kwenye hoja kuntu uliyoanza nayo.

Vijana Punguzeni uchumia siasa kidogo ili jamii ipate kuwaelewa kwa Mambo mhimu kama haya.
 
Kwa kweli huu ni ubabaishaji!

Japokuwa huenda wana sababu za msingi kama walivyozitaja, lakini inaonesha ni jinsi gani walivyo na roho chachu!

Yaani kajisababu kadogo tu tayari mkopo umefyekwa!

These people bwana! Doooh!
Unanifurahisha na dp ako hapo mkuu!
 
Alieshiba hamjui mwenye njaa...tuliotoka kaya masikin mungu anajua
 
Tukiweka ushabiki pembeni wanachokieleza bodi kina mantiki isipokuwa walitakiwa waeleze ili mapema au watumie busara kutokana na hali halisi.

Sababu hiyo hela ya kujikimu inalipwa kwa siku x idadi ya siku za mhula wa masomo. Kwa mfano kama muhula wa masomo una siku 60 na wanalipa 7,500 kwa siku maana yake watalipa 7,500 x 30. Hivyo kuongezeka au kupungua kwa siku za masomo kutaathiri kiwango cha pesa pia.

Ingawa sasa kutokana na hali halisi ya kipindi hiki, na ukweli kwamba kunaweza kuwa na matumizi ya ziada kwa ajiri ya kujikinga wangeweza kuwalipa tu kwa viwango vya siku za kawaida ili kiwasaidia vijana ukizingatia na ukweli kwamba bajeti ilishapitishwa.

Tatizo la awamu hii, unaweza kuona bodi wanataka kusave hizo hela alafu warudishe kwa mkuu kwamba zimebaki, afadhali mkuu keshatoa ujumbe kupitia TAKUKURU watendaji wake waache kujipe.. ndkz
 
Hivyo siku zikipungua na ada inapungua? au siku wasizoenda shule hawatakiwi kula? au kulala kwenye hostel au nyumba za kupanga wanazozilipia?.
Kweli ccm mbele kwa mbele.
 
So unachotaka kusema kama walikua wanakula Mara tatu kwa siku na masaa ya kusoma yameongezeka basi chakula nacho wale Mara nne au tano kwa siku si ndio???

TANZANIA DOUBLE STANDARD KILA MAHALI.
 
Kwani wamewakata mpaka stationeries ?
Coz km masaa yako Yale Yale baasi stationary isikatwe. Labda ya msosi sawa. Lkn all in all wawape tu full boom waji enjoy banange
 
Hongera sana kwa mchango mzuri sana kwa kuwatetea wadogo zetu na watoto wetu pia
 
100% wako Sawa, pesa zinalipwa kwa idadi ya siku za masomo.. Mbona iko wazi.
 
Chadema wapingaji, eti nalo hili ni mtaji wa kisiasa! Sasa siku zimepungua unataka ulipwe zaidi kutoka wapi? Chadema mngejikita kutangaza Sera zenu sio kudandia hoja, tar 28 kipigo kiko pale pale lazima mnyampe tu!
 
Ebu HELSB ishaurini serikali iondoe retention fee ya asilimia 6, hii inawafanya wanufaika kuwa watumwa na mkopo kutolipika.

Aidha ishaurini pia serikali kupunguza riba/makato na yawe ya asilimia 8/7 kama ilivyokuwa awali. Kuongezeka kwa makato imekuwa mwiba kwa wanufaika hasa ukizingatia wanufaika wengi ni watumishi ambao tangu 2015 wamekuwa wakiishi kwa kulipwa mishahara ile ile ya 2015 wakati Hali ya maisha inabadilika kila kukicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…