HESLB imetoa siku nne kwa Wanafunzi 2,982 walioomba mikopo kwa mwaka 2021/2022, kukamilisha taratibu za maombi yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
HESLB YATOA SIKU NNE WAOMBAJI KUFANYA MAREKEBISHO

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa muda wa siku nne kuanzia Oktoba 4-7, mwaka huu kwa wanafunzi 2,982 walioomba mikopo kwa mwaka 2021/2022 kufanya marekebisho ili kukamilisha taratibu za maombi yao.

Ili kupata taarifa za kina kuhusu marekebisho hayo, waombaji husika wameshauriwa kutembelea akaunti zao walizotumia kuomba mkopo kwa njia ya mtandao maarufu kama SIPA-Student’s Individual Permanent Account (SIPA).

Akizungumza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo HESLB, Dkt. Veronica Nyahende alisema mara baada ya kukamilika kwa hatua hiyo ya marekebisho, HESLB itaanza kuwapangia mikopo wanafunzi wahitaji.

“Katika uhakiki wa maombi tumebaini waombaji 2,982 fomu zao zina kasoro. Tumetoa muda wa siku nne, na baada ya hatua hiyo kukamilika tutaanza mchakato wa kupanga mikopo kwa wanafunzi wenye sifa na uhitaji”, alisema Dkt. Nyahende.

Kwa mujibu wa Dkt. Nyahende waombaji pia watapaswa kutembelea akaunti za SIPA ili kupata taarifa za mikopo watakayopangiwa na HESLB baadaye mwezi huu.

Hadi kufikia Septemba 30, mwaka huu, HESLB ilikuwa imepokea maombi 88,688 na kati ya maombi hayo; 85,706 yalikuwa kamilifu na 2,982 yalitakiwa kufanyiwa marekebisho.

Dkt. Nyahende aliongeza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha fedha za mikopo ya wanafunzi zinalipwa kabla ya vyuo vya elimu ya juu kuanza kufunguliwa kuanzia Oktoba 25 mwaka huu.

Katika mwaka wa masomo 2021/2022, Serikali imetenga kiasi cha TZS 570 Bilioni kwa ajili ya bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu 162,000 wakiwemo wanafunzi 62,000 wa mwaka wa kwanza na 98,000 wanaoendelea na masomo.
DKT.VERONICA NYAHENDE.JPG

Mkurugenzi Upangaji Mikopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Veronica Nyahende
 
Ivi ukiingia kwenye akount yako utaona viashiria gani vinavyooneaha umekosea...
 
View attachment 1963933
Mkurugenzi Upangaji Mikopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Veronica Nyahende
kujua kama form yako imekosewa, unajuajaje sassa ?, au kama majina ya waliokosea form zao, yako wapi,?
maana huu umekuwa mkanganyiko madogo wanahaha, na kweye account zao hawakuti taarifa yoyote ya nini kinamiss kwenye form zao
 
Back
Top Bottom