HESLB na NIDA kushirikiana kuwatambua waombaji mikopo kupitia NIN

HESLB na NIDA kushirikiana kuwatambua waombaji mikopo kupitia NIN

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) leo Ijumaa Mei 16, 2025, wamefanya kikao na waandishi wa habari katika ofisi za HESLB Kanda ya Mashariki zilizopo Dar es Salaam kwa lengo la kuutarifu umma kuhusu kuanza kushirikiana kuwapatia namba ya utambulisho (NIN) wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026.

Akiongea kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia, ameweka wazi kuwa namba ya utambulisho wa taifa itakuwa ni ya lazima katika kuomba mkopo kwa mwaka ujao wa masomo. “Tunatarajia kufungua dirisha la maombi ya mkopo mwezi Juni, 2025… kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 … namba ya utambulisho wa taifa itakuwa hitaji la lazima katika kujaza fomu za maombi ya mkopo, hivyo waombaji wote wanapaswa kuwa na namba hii wakati wa kujaza maombi yao ya mkopo”, amesema Dkt. Kiwia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. James Kaji, amesema kuwa NIDA wapo tayari kuwahudumia wanafunzi wote wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu na kuomba mikopo kutoka HESLB kwa kuwapatia namba za utambulisho kwa wakati na hivyo wanafunzi wanapaswa kufika kwenye ofisi za NIDA mapema ili kupatiwa namba za utambulisho.

“NIDA ni maisha, kwa sasa … NIDA inaendelea kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mifumo yote ya serikali inasomana… tunawasisitiza waombaji wote wa mikopo ya elimu ya juu kuhakikisha wanafika mapema NIDA ili kupata namba ya utambulisho wa taifa”, ameeleza Bw. Kaji.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kiwia amesisitiza umuhimu wa matumizi ya namba ya utambulisho kwenye uombaji mkopo kuwa itasaidia kupata taarifa za uhakika za waombaji mikopo na katika urejeshaji wa mikopo ya wanafunzi mara wanapohitimu elimu zao. “Tayari wataalaamu wetu wa mifumo kutoka HESLB na NIDA wamekalimisha kuunganisha mifumo, ili kuhakikisha waombaji wote wa mikopo wanajaza namba za utambulisho katika maombi yao ya mkopo, na kupata taarifa za uhakika za waombaji mikopo ambazo pia zitasaidia katika urejeshaji wa mikopo”, amesisitiza Dkt. Kiwia

Kuhusu kurahisisha huduma kwa waombaji wa namba za utambulisho wa taifa, Bw. Kaji amesema NIDA imeboresha huduma kwa njia ya mtandao na kusisitiza waombaji wa namba za utambulisho wa taifa (NIN) kuingia kwenye mtandao wa NIDA kwa kutumia kiunganishi https://eonline.nida.go.tz ili kuwasilisha maombi yao.

“Waombaji wa namba za utambulisho wa taifa wanaweza kuomba kupitia mtandapo wa NIDA…njia hii ya mtandao inarahisisha sana na kupunguza foleni kwenye ofisi za NIDA kwa kuwa 75% ya usajili inafanywa na mwombaji mwenyewe kupitia njia ya mtandao na 25% itafanywa na ofisi ya NIDA”, amefafanua Bw. Kaji.

HESLB na NIDA wamejipanga kuanza kutoa elimu kuhusu umuhimu na namna kupata namba ya utambulisho wa taifa kwa kuanza na mkoa wa Dar es Salaam ili kurahisisha zoezi la kutoa namba kwa waombaji wa mikopo wanaotarajia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka 2025/2026.
 
Mimi naomba kuwasilisha changamoto na kupata utatuzi! Kama ilivyotangazwa na bodi ya Mikopo elimu ya juu bila Nida hakuna mkopo, Kuna changamoto ya kutofautiana majina ya vyeti vyao masomo na nida kwa baadhi ya wahitaji wa mkopo kutokana na sababu mbalimbali.

Kutokana na Changamoto hiyo, baadhi ya wahitaji katika mkoa wa Dodoma wamekutana na changamoto ya kutopata huduma ya kuendelea na hatua za kubadilisha majina ya Nida ili kuwiana na ya kwenye vyeti kwa wakati wakifika katika ofisi za Ardhi.

Changamoto kubwa ni Mtoa huduma mkuu katika ofisi za ardhi amekuwa akitumia lugha kali kwa wateja, kupoteza muda kwa kuongea na simu huku foleni ikiwa kubwa na ukifika muda wa kufunga ofisi anawaambia waje kesho napo inakuwa hali ileile.

Hivyo tunaomba mamlaka husika iwasaidie wahitaji ili waweze kumaliza haraka zoezi la kubadilishana majina waweze kuwahi kuomba mkopo kwani mtoa huduma mkuu idara au ofisi za Ardhi mkoa wa Dodoma Madamu huyo hajali kabisa hali ya wateja bali amekuwa akiwafukuza na kuwatoa nje ya ofisi kwa ukali na kuzingatia Dirisha la mkopo karibuni kufunguliwa na watoto wa masikini wanahitaji kuomba mkopo ili nao watimize masomo yao na ndoto zao.

Naomba changamoto hii ifikishwe kwa wahusika iweze kutatuliwa mapema.

Ahsanteni na Mungu akusimamieni
 
Kuna ugumu na sintofahamu sana katika hili.Hapo kwenye kipengele cha NaPA zoezi ni gumu jamani ifanyike namna rahisi.
 
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu tuoneeni huruma watanzania jamani.Hiki kipengele Cha kuweka BARUA ya UTAMBULISHO tena kutoka huko kwenye app ya NaPA imekuwa ni changamoto sana.kwani;
1.Watu wengi hawana kumbukumbu za taarifa zao walizotumia kujaza wakati wa zoezi la anuani za makazi.Hata hivyo taarifa ziliwekwa za wenye nyumba na kama mtu ni mpangaji inakuwa ngumu kuzipata hizo taarifa hata akienda Kwa mtendaji wa Kijiji kufuatilia.
2.Watendaji nao hawaelewi kitu hata ukifika kuuliza.
3.Muda unaotumika ni mkubwa kuzunguka huko.

NB: Mambo ya postikodi,namba ya nyumba kulazimika kuwekwa ni usumbufu na changamoto pia.

NADHANI MATUMIZI YA NIDA NDO YANGEKUWA KILA KITU NA SULUHISHO KWA WAOMBAJI,WAZAZI NA WADHAMINI.KWANI NIDA INA KILA KITU NA TAARIFA ZOTE ZA WAHUSIKA.INGETUMIKA HII NA HAYO MENGINE ONDOENI YAMEKUWA KIKWAZO NA NGUMU KUFANIKISHA UOMBAJI.WENGI TUMEKWAMA,TUNAOMBA MSAADA TAFADHARI.
 
Back
Top Bottom