HESLB, naomba kupata maelekezo juu ya allocations za fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo(Field)

HESLB, naomba kupata maelekezo juu ya allocations za fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo(Field)

P Accountant

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2020
Posts
371
Reaction score
182
Habari za wakati huu kwenu.

Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ukuu wake na rehema tele atupazo katika maisha haya.

Nimekuja hapa, nikiamini nitapata msaada na ushauri wa kimawazo juu ya suala tajwa hapo juu.

Ipo hivi, mnamo mwaka 2020 bodi ya mikopo elimu ya juu (HESLB) ilifanya allocations ya fedha za kujikimu kwa wanufaika wa mkopo, na kuonesha mgawanyo wa fedha kwa kila mwaka wa masomo, nikiwa na maana:

2020/2021
2021/2022
2022/2023 kwa wanafunzi wa miaka mitatu ya masomo.

Katika allocations hizo, baadhi ya wanafunzi ambao hawakuwa na field mwaka wa kwanza hawakuwekewa allocations za field, lakini allocations ziliwekwa kwa mwaka husika wa field 2021/2022, ambao ndio mwaka huu.

Mshituko ulikuja kutokea pale bodi ya mkopo(HESLB) kubadirisha allocations kwa mwaka wa pili wa masomo, na kuweka allocations kama ya mwaka wa kwanza wa masomo, yaani allocations zisizo na fedha za field.

Muda unaenda, na siku zinajongea taratibu kuelekea wakati wa field. Hatujui hatima ya fedha tulizowekewa(allocations) za field na baadae zimeondolewa.

Maswali yangu
√Nini hatima ya fedha zile kwetu wanafunzi.
√Kwa wale ambao mmewahi kupitia changamoto hii ilikuwaje muafaka wake.

Naamini nitajifunza kwa mawazo bora toka kwenu.

In God, I trust.

Nawasilisha mada tajwa juu.
 
Mods, naomba mpeleke Uzi kwenye jukwaa la habar na hoja mchanganyiko.
 
We tulia tu hizo ndio hazirudi tena, tafuta namna nyingine ya kuishi kipindi utachokua field [emoji3][emoji3]
OK, vizuri. Ilipaswa watoe maelekezo juu ya hili. Almost UDSM yote wanafunzi ambao hawakuwa na allocations ya field first year, wameondolewa allocations second year. Ni ajabu na inatia wasi wasi.
 
Back
Top Bottom