tamuuuuu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 22,779
- 31,297
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu tuoneeni huruma watanzania jamani. Hiki kipengele Cha kuweka BARUA ya UTAMBULISHO tena kutoka huko kwenye app ya NaPA imekuwa ni changamoto sana. kwani;
1. Watu wengi hawana kumbukumbu za taarifa zao walizotumia kujaza wakati wa zoezi la anuani za makazi. Hata hivyo taarifa ziliwekwa za wenye nyumba na kama mtu ni mpangaji inakuwa ngumu kuzipata hizo taarifa hata akienda Kwa mtendaji wa Kijiji kufuatilia.
2. Watendaji nao hawaelewi kitu hata ukifika kuuliza.
3. Muda unaotumika ni mkubwa kuzunguka huko.
NB: Mambo ya postikodi, namba ya nyumba kulazimika kuwekwa ni usumbufu na changamoto pia.
Nadhani matumizi ya NIDA ndio yangekuwa kila kitu na suluhisho kwa waombaji, wazazi na wadhamini. Kwani nida ina kila kitu na taarifa zote za wahusika. Ingetumika hii na hayo mengine ondoeni yamekuwa kikwazo na ngumu kufanikisha uombaji. Wengi tumekwama, tunaomba msaada tafadhari.