digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,508
- 23,368
Mkuu nimekufuatilia sana naona kama unahusika na haya mambo ya NaPa huko Helsb,lakini ni Mfumo mgumu sana huu na sidhani kama kitapatikana mnachokilenga.nida haina location, taarifa za napa pia zipo online ukizitaka unarequest unatumiwa code kwny simu yako unatumiwa mzigo wako wote unausoma, kitu kingine hukijui ni kuwa anayeupdate taarifa za nida upo naye mtaani kwako, kitu chcht hakipo sawa unamfata tu mtendaji anakurekebishia..so mzee haupo sawa
Huwezi Tengeneza Mfumo kwa lengo ka kujua location ya mkopeshaji wako ambaye unategemea kuja kumudai baada ya miaka 3-5, yeye siyo jiwe au mtu kwamba utamkuta pale pale.
Pili kama ni location ya wale mnaowadai,vipi walioko kwenye nyumba za kupanga mtaweza kweli kuwapata maana watu wanahama Kila kukicha,ndani ya mwaka Mmoja mtu anabadili makazi mara tatu.
Ninavyo ona Huu Mfumo umelenga kupunguza idadi ya waombaji wa mkopo kulingana na usumbufu uliopo wa kupata NaPa,Mimi nimeomba namba ya utambulisho Leo ni siku ya nne sijapata,nilitegemea nikiomba hiyo namba ije pale pale bila usumbufu, lakini nikusubiri kwa Muda mrefu.
Hoja ya NaPa ni nzuri lakini tujipe muda,isiwe kigezo muhimu ili kupisha utatuzi wa changamoto zilizopo.