....Hawa jamaa wanazuia watu kujua matumizi makubwa sana ya bangi likiwemo lile la kutibu cancer na badala yake wanajifanya kukubali kwamba kweli bangi ina faida lakini wanataja faida ndogondogo tu,kubwa hawazitaji na hata wakizitaja watakwambia bado hazijakuwa proved,..............
Kati ya mambo rahisi sana kujua ukweli wake,bangi ni mojawapo,ukiamua tu kujua ukweli wa bangi wala haipiti wiki moja utakuwa umejua kila kitu..........
Kuhusu bangi,nitatoka kidogo nje ya mada kwa kuwa nataka kuzungumzia jambo muhimu sana ambalo ni vyema mkalijua pia.
Mojawapo ya mambo muhimu sana duniani ni NISHATI/ENERGY.Hakuna mtu yeyote ambaye anapingana na hili.Sasa hivi tunasikia vita kubwa maeneo mbalimbali ya dunia yetu,sababu mojawapo kubwa inayosababisha vita hivyo ni vyanzo vya nishati kama vile petroleum/crude oil/gas.Petroleum ni mojawapo ya malighafi inayotumika kuzalisha DIESEL na PETROL.Kwa hapa nitazungumzia DIESEL.
DIESEL ni mojawapo ya chanzo cha nishati kitumikacho maeneo mbalimbali ikiwamo vyombo vya usafiri na mitambo ya kuzalisha umeme.DIESEL huweza kupatikana baada ya kufanya utaratibu wa kikemikali kutoka kwenye PETROLEUM,SYNTHESIS GAS na ANIMAL/PLANTS/VEGETABLE OIL.Hivyo kutokana na utaratibu wa upatikanaji wa DIESEL,tunaweza kuita DIESEL majina ya aina tatu lakini yakimaanisha DIESEL hiyohiyo ila utaratibu wa upatikanaji ni tofauti,majina hayo ni PETROLEUM DIESEL,SYNTHETIC DIESEL na BIODIESEL.
Hapa nitazungumzia BIODIESEL.BIODIESEL ni diesel ambayo hupatikana baada ya kufanya utaratibu wa kikemikali kwenye vegetable oil/mafuta ya mimea au fats za wanyama/animal fats(biolipids).Hapa nitazungumzia zaidi vegetable oil.Kuna vegatable oils nyingi sana ambazo huweza kufanyiwa utaratibu wa kikemikali ili kupata BIODIESEL,mfano,canola oil,soy oil,corn oil,sunflower oil,hemp seeds oil nk.Hapa nitazungumzia HEMP/MARIJUANA SEEDS OIL.
HEMP/MARIJUANA/BANGI ndio mmea wenye uwezo wa kuzalisha BIODIESEL kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko mimea yote duniani kutokana na tafiti zilizokwishafanywa.HEMP/BANGI ina uwezo wa kuzalisha hadi mapipa/barrels 30 ya BIODIESEL kwa ekari moja ya HEMP/BANGI.PIPA/barrel moja lina ujazo wa lita takribani 119,hivyo basi kwenye ekari moja tunaweza kupata takribani lita 3,500 za BIODIESEL.Nadhani mnaweza kufikiria wenyewe lita hizo ambazo ni ekari moja tu zinaweza kuzalisha umeme kiasi gani kwa siku au zinaweza kuendesha magari mangapi kwa siku maeneo ya mijini.
BIODIESEL hupatikana kwa utaratibu wa kikemikali uitwao TRANSESTERIFICATION ambapo vegetable(hemp) oil(around 54 degree celcius) inapambanishwa na alcohol(eg methanol+catalyst) na kupata BIODIESEL pamoja na mabaki ya GLYCERIN,glycerin pia huweza kutumika kuzalishia sabuni,shampoo nk.Hii sio miujiza ndugu zangu,ni ukosefu wa uelewa tu ndio unaowafanya wengi washangae,elimu hii hatuwezi kuipata darasani,na hata ikifundishwa lazima mwishoni waweke disclaimer kwamba eti "biodiesel itakayozalishwa na bangi ni kidogo sana kiasi cha kutokuwa na maana yoyote kuhangaika nayo kuizalisha",huu ni uongo mtupu,wanasema hivi ili kuwarubuni watu wasijishughulishe nayo lakini ukweli ni kwamba bangi ni mmea wa ajabu sana na wenye manufaa makubwa sana watake wasitake.Na ndio maana wanapiga vita uzalishaji wa bangi kwa kisingizio cha kwamba bangi ni madawa ya kulevya.Ukweli ni kwamba bangi ni hatari sana kwenye biashara zao za mafuta na gas pamoja na tiba ya cancer ambayo tumeshaizungumzia.
Biodiesel process:
Utaratibu wa kikemikali unaohusisha mlinganyo wa kikemikali mnaweza kuupata kwenye mitandao,sina haja ya kuuweka hapa,lakini unahusisha organic chemical reactions,kwa wale ambao wamepitia vizuri organic chemistry wanaweza kuelewa kiurahisi.
Hapa sasa nadhani mnaweza kupata picha ya sababu halisi kwa nini bangi imeharamishwa.Wengi mtajiuliza,kwa sasa hawatumii bangi kuzalisha diesel kama kweli ina faida kama hii?Jibu lake ni kwamba kutakuwa hakuna tena monopoly ya biashara ya mafuta na hasa diesel,kila mtu anaweza kuzalisha diesel kama atapenda na hivyo kufanya diesel isiwe suala kubwa ki hivyo kama linavyochukuliwa sasa na hivyo bei yake kushuka.Mambo haya ndio hawa jamaa hawayataki,wako tayari kuvamia hata kijeshi nchi yoyote itakayozalisha bangi katika large scale kwa matumizi hayo,kama watagundua hilo.
Hebu angalia hapa uone jamaa anavyozalisha BIODIESEL ili uone kwamba hili suala sio big issue.Pia fahamu kwamba biodiesel ina faida nyingi zaidi kuliko petroleum diesel.Lakini hapa chini hawatumii bangi.
https://www.youtube.com/watch?v=aOzWgyB1FSk
https://www.youtube.com/watch?v=TC9h78b2RM4 (angalia part 1 na part 2)