Habari wana JF, hii video nimeirekodi kwa mikono yangu mwenyewe, inaonesha Barabara ya Dodoma to Iringa jinsi ilivyo hatarishi kwa maisha ya watu wanaotumia, barabara ina viraka vingi na mahandaki mengi sana.
Nimeiangalia kwa jina la kizalendo na kugundua kuwa hii barabara inahitaji matengenezo makubwa.
Barabara hii ni mzigo kwa Serikali na walipa kodi.
Mbaya zaidi Wakala wa Barabara - TANROADS Dodoma wao wanachimba wanajaza udongo wanaondoka, tofauti na upande wa Iringa ambao wao wanaziba mashimo na wanajitahidi ku-maintain barabara.
Wananchi tumelalamika sana kuhusu hii changamoto, ukiangalia hapo kwenye video utaona jinsi gani ambavyo dereva unahitaji kuwa makini, la sivyo unaweza ajali ni nje-nje au kuharibu magari.