Hii chapati niliyotengeneza, usipokua makini utajing'ata Vidole

Umewaza kiutu uzima. Wewe una akili sana mkuu.
 
Hongera kwa uthubutu,punguza mafuta tho. Mengine yote kamaliza culture gal,kazi kwako
Asante mkuu wangu wa kazi. Nitazingatia yote ulionishauri. Asante pia kwa kitumia muda wako kunielekeza.
 
Asante mkuu. Ile ya kusukuma sina tatizo. Sababu nanyunyuzia mafuta kidogo na kijiko huku naigeuza hadi inaiva. Tatizo na kuitengeneza iwe ya duara. Chapati nikisukuma umbo lake ukaona picha. Unaweza cheka hadi mbavu ziume.

Nanunua zile za dukani mi napasha moto tu.

Wewe kwa mapishi upo Vizuri. Ila kwa sasa hutanitisha chochote sababu hadi urudi, utakuta nshakua mtaalam sababu nimepata wadhamini wa mapishi. Mzigua90 ndani ya nyumba. Nataka nikufunike.

Nikishajua kuoa ntafikiria, nikiulizwa naoa lini ntakua najibu bado nipo nipo kwanza.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tufuge kwa nyumba zipi mkuu? Tunanunua sokoni wale fresh kabisa. Kufuga nyumba zetu za kupanga hizi nafasi ndogo
Shida yake tulale na nnya ya kuku vitandani,mana sie wengine ni kama tunaishi stoo
 
Chapati zote lazima niweke sukari kiduchu na chumvi kiduchu yaan kama hakuna sukari sijui nazionaje walai.
Mi hapana sukari kweny chapati naweza rudisha chenchi,yupo shoga ye mpaka za kusukuma anatia sukari,na za maji hatii chumv ni sukari tu uwiii
Sukari imenishinda kwenye chapati ya maji.
Naonaga inanoga ukiblend yai unga na chumvi. Ukishapata rojo ndo ukate kate kitunguu hoho na carrot unaikwangua.
 
Hiyo mingano iliyofinyangwa kwa pamoja ndo unaiita chapati? Acha dharau mkuu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hahahaaa... Huwezi elewa utamu wake hadi uonje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…