Hii confidence ya kununua nyumba za watu na kuzifanya makazi mnapata wapi?

Hii confidence ya kununua nyumba za watu na kuzifanya makazi mnapata wapi?

Vipi kuhusu magari ya mtumba/used?
Kuna magari yananuksi pia. Ila kwa mjapani uongo, uchawi hauvuki maji, shida ukinunua gari la M'bongo!
 
Niliwahi panga nyumba Magomeni Mwembechai Jiran na ilipokuwa DDC Magomeni.
Kila mwaka mwenye nyumba analeta shehe kuagua wapangaji wake.
Anakuja na ubani na kioo kikubwa anapita kila vyumba kumkagua Mpangaji.
Na kuna vitu walikuwa wanazika getini anapopita kila mtu.!
Si shauri mtu kununua nyumba.
 
hamna cha kukukuta wala nini,kwani sisi tusioamini uchawi, tunaishi mbinguni ambako hamna uchawi?...hatuangaiki na mazindiko ya nyumba wala mashamba ilihali majirani kutwa kukesha na wachungaji na waganga miaka nenda rudi, na hamna wanachoambulia.....acheni huo ujinga wa fikra duni🚮🚮
sawa nakupa ushindi mkuu
 
Back
Top Bottom