Hii faulo ya Djuma Shabban ni Red Card (Lefa kapeta)

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Your browser is not able to display this video.


Imeniuma sana tena sana. Mchezaji professional kama Djuma anacheza mchezo wa akina Ninja. Michezo ya kishamba ni ya kukemea katika soka la waungwana.

Yaani Football umegeuka uwanja wa ndondi. Halafu refa kapeta tu. Huu uhuni hautakiwi kufumbiwa macho.
 
Huu ni uzi wa ngapi unaanzisha kuhusu yanga ndani ya dk 30 tu?

Muangalieni huyu jamani asije kujitundika.
Sasa unataka nianzishe uzi wa timu gani wakati matukio ya leo yalikuwa ni Yanga. Mbona unataka kuninyima haki yangu ya kuchangia hapa JF. Wewe hujakatazwa.
 
Kkufupi hujawahi kucheza mpira kabisa
Kama umewahi ungejua kwanini wachezaji wanafanya hivyo kama djuma.
Japo sio kitendo cha uungwana..
Mzee, acha kutetea michezo ya hovyo hovyo. Mahaba weka pembeni. Unampiga mchezaji ngumi ya pua huoni unaweza kuua kabisa!?
 
Sasa unataka nianzishe uzi wa timu gani wakati matukio ya leo yalikuwa ni Yanga. Mbona unataka kuninyima haki yangu ya kuchangia hapa JF. Wewe hujakatazwa.
Nilivhokiona ni kwamba Mwamuzi alikuwa mbali na mchezo ilisimama Kwa ajili ya mpira wa kurushwa. Lineman alipomyoosha kibendera ndo matukio yote mawili ualipoyokea.

Kwa maoni yangu kulikuwa na Kadi mbili nyekundu moja Kila upande. Japokuwa kitendo alichofanya Djuma si cha kiungwana lakini alichofanya beki naye ni faulo ya kijinga.
 
Nilivhokiona ni kwamba Mwamuzi alikuwa mbali na mchezo ilisimama Kwa ajili ya mpira wa kurushwa. Lineman alipomyoosha kibendera ndo matukio yote mawili ualipoyokea...
Beki ya Police alifanya nini!?. Djuma ameshindwa kucheza mpira kwa sababu ya uzee wake analeta michezo ya ngumi.
 
LEFA ni mnyama gani we Vannesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…