Angalia ufaulu wa NECTA wa shule, huko wanapotoka wenye "meno yaliyooza" dhidi ya kule wanapotoka meno meupe.
IQ inapimwa kwa kufaulu NECTA???? 😅, aisee bado tunasafari ndefu sana kama bado kunawatu mnadhani hiyo mitihani ya serikali zetu ndio kipimo cha akili.
Ingekuwa hivyo basi nchini tungekuwa na akina Elon musk wengi, kina mark Zuckerberg wengi, wagunduzi wa technolojia wengi, wagunduzi wa madawa&vifaa tiba wengi.
Moja kati ya siraha za kuharibu IQ kwa Afrika/Tanzania ni hizo takataka za Colonial education/elimu yetu kuanzia msingi mpaka huko vyuo vikuu, huko ambako unafunzwa kuukataa ukweli na kuyakubali maandishi/nakala za wengine zilizopitwa na wakati zitumike karne hii, huku mtoto akiwekewa wigo wa kuwaza/kufikiri nje ya box/ kupangiwa kipi cha kuamini na kukalilishwa mambo yasiyo na msingi.
La pili, Dunia nzima inaongozwa kwa misingi na mipango ya watu waliyoisuka ili wautawale ulimwengu vile wanavyotaka
Na njia za kumtawala mtu asikiuke sheria zao/kuwapinga/kwenda kinyume na mfumo ndipo wakaintroduce mifumo ya kucontrol mienendo ya kila mwanadamu automatically anapozaliwa mpaka anakufa anakuwa chini ya mifumo hiyo kwa kutaka ama kutotaka, ukijaribu kwenda kinyume na mifumo ndipo unaitwa mshamba/mjuaji/ama unakosa zile basic needs&social interaction/social services kwa sababu ya kwenda kinyume na mifumo (elimu,dini, afya).
Mfano wa mifumo ni DINI, yaani hii ndio njia kubwa ambayo mtoto tangu anazaliwa anajazwa hofu&stories za kufikilika ili awe mtiifu kwa serikali yake na sheria za utawala kupitia kutulizwa kiroho/nafsi mpaka kimwili kutokana na mafundisho anayolishwa na hao viongozi wao wa kidini ambao nao ni puppets wa serikali/secrets societies.
Mfumo wa Afya, hapa ndipo pabaya zaidi maana kwa %kubwa ya watu tumeshalishwa sumu nyingi mpaka sasa kiasi kwamba huwezi kwenda nje ya mfumo tumewekewa utegemezi mkubwa kwa madawa/chanjo artificial zinazoharibu uwezo kwa akili kuwaza vizuri huku tukiendelea kuaaminishwa hizo tiba za kisasa ni nzuri.
Mifumo ya uchumi, hapa hata sipaongelei kabisa maana kila mtu anajua.
Mifumo ya kijamii&Sanaa, hapa haswa kwa mtanzania ndipo tumekamatika vibaya sana, hata ukikaa na vijana ambao walitakiwa kuwa tegemezi kwa taifa stories zao kutwa nzima ni mpira/simba&yanga sijui mambo ya akina arsenal na upuuzi kama huo,
kuna wengine mpaka wanapata uraibu wa betting kisa huu ujinga ulioingia ktk fikra zao, hii nayo ni aina ya kumcontrol mtu muenendo wake na maisha yake yaende vipi, awaze nini ,yaani mtu anapoamka mpaka anapolala anakuwa kautumikia mfumo wa kumtawala kwa 100%, imagine mtu anaamka huyo kashika simu, chaamaana anachotizama ni hizo takataka za simba&yanga, akihama sana anatizama miziki isiyo na maana zaidi ya kusifia ngono na kuvunja maadili, akitoka hapo labda ataenda kazini/kibaruani ambako nako huko anakutana na makondoo wenzie, na storie zao ni zile zile za kuwatala aina ipi ya kuwaza/kufikiri, utawaona watu kazini storie zao ni zile zile sijui simba kamfunga nani, Madrid kafanya usajili upii, yaani jitu linajua ratiba nzima za match kuliko kujua ratiba za viongozi wake serikalini
Jitu linajua majina ya wachezaji zaidi ya 20 maajabu haliwezi kutaja hata mbuga 5 za wanyama/vivutio vya utalii nchini, wala halijui data za maendeleo ya nchi yale, ila umkute kwenye mpira sasa.
Hili halijaisha, mtu huyu huyu ambaye kazini na nyumbananawaza yale yale na bado mpaka siku za mapumziko(weekend) utamkuta anatumbukia kwenye aina nyingine ya kutawalika kiakili yaani anakwenda kule kule alikoaminishwa tangu utotoni kuwa ni sehemu ya kumjua Mungu (kanisani/msikitini) huko utakuta anamalizia weekend yake then week mpya inendelea na CIRCLE ile ile ya kuutumikia utumwa wake.
Kwa namna hii bado tutaendelea kutawalika na kuzalisha vizazi vya mitoto mipumbavu/mijinga isiyoamini ktk kujitegemea zaidi ya kutegemea wengune ndiomaana hii nchi haiamini kama mtanzania anaweza kujilietea maendeleo pasipo mikopo ya mzungu/mchina
Dalili mojawapo za kujua kuwa tunatawalika/tupo under control ya kifikra ni aina hata ya mawazo ya watu humu mnaona komenti zao zimejawa matusi, lugha chafu, kupinga mada za watu bila kuleta hoja, kufuata mkumbo, kuendekeza mambo ya kijinga.