Hii haifai, Waziri wa OR Tamisemi anamkusanyia fedha Rais Samia ili agombee 2025 akiwa anafanya shughuli za kiserikali sio za kichama

Hii haifai, Waziri wa OR Tamisemi anamkusanyia fedha Rais Samia ili agombee 2025 akiwa anafanya shughuli za kiserikali sio za kichama

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Tamisemi_mchango_Samia.png

BODABODA WAMCHANGIA RAIS SAMIA 3,170,000/= ZA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2025

Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amepokea mchango wa shilingi 3,170,000/= wa madereva bodaboda nchini, walioutoa kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa ajili ya kumuwezesha kuchua fomu ya kugombea urais mwaka 2025 baada ya kuridhishwa na uongozi wake.

Mhe. Mchengerwa amepokea mchango huo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na bajaji wa jiji la Dar es Salaam.

“Leo nimeshuhudia na kupokea mchango wenu wa kumuwezesha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais mwaka 2025 kwa mapenzi yenu wenyewe, bila kushurutishwa na hii ni kwasababu Rais Samia ameingia katika mioyo yenu na watanzania wengine kutokana na uongozi wake imara,” Mhe. Mchengerwa ameeleza.

Mhe. Mchengerwa amesema, uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umegusa mioyo ya madereva boda boda, wakulima, wafanyakazi na kila mtanzania, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ana sababu ya kumuunga mkono kwa vitendo kwa kumchangia ili aweze kutimiza azma yake ya kuendelea kuliongoza taifa na kuliletea maendeleo.

Waziri Mchengerwa amewapongeza viongozi wa boda boda kutoka katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Mwanza, Geita, Katavi, Iringa, Mbeya, Songwe, Rukwa, Lindi,Tabora, Dar es Salaam pamoja na Zanzibar kwa kuwasilisha michango yao ya kumuwezesha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kuombea urais mwaka 2025.

“Fedha hizi 3,170,000/= mlizo changa na kunikabidhi, nami leo hii hii nitakwenda kuzikabidhi kwa Mhe. Rais ili atambue namna ambavyo mna muunga mkono kutokana na kuthamini uongozi wake madhubuti na imara,” Mhe. Mchengera amesema.

Waziri Mchengerwa ameahidi kuwa, Serikali itaendelea kuthamini mchango wa madereva boda boda na bajaji wanaoutoa katika maendeleo ya taifa.

Chanzo: Ukurasa wa Tamisemi mtandao wa X
 
Huu ujinga tukiulea nchi itabaki mifupa mitupu. Waliochanga wajinga ,aliyepokea mjinga anayechangiwa jitu la hovyo na halifai
ccm kuna ujinga inaulea na unazidi kukita mizizi naamini kabisa hii hali ikukumbatiwa bila kukemewa huko mbeleni watajaribu kurudi watu kwenye misingi sahihi itakuwa ni ngumu na kuna uwezekano mkubwa kizazi kijacho kikashangaa namna ujinga ulivyokaliwa kimya na kizazi cha sasa.

Muda utafika tu

Hizo mambo zikifanywa na upande ule hata msajiri na mlezi wa vyama na huyo huyo Mchengerwa utawaona wanavyobwatuka.
 
Siyo BODABODA sema MAAFISA USAFIRISHAJI
 
Hao sio bodaboda, ni ma uvccm yamefanya maigizo!
Huyu mama uongozi wake ni zaidi ya dhaifu ndio maana wahuni wanahangaika sana aendelee kubaki madarakani yatafune zaidi nchi!
 
Back
Top Bottom