ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,850
- 6,030
Tanesco wameshashindwa kuhudumia! Dawa ni kuruhusu makampuni mengine yaanze kusambaza umeme!!Umeme kwa huu mwezi unakatika Sana siku nzima, ukiuliza emergency wanajibu matengenezo, nimetembea mikoa Saba mwezi huu shida Ni hiyo hiyo, huku wengine wanasema mitambo imechakaa , huku wengine wanasema stigler, wengine wanasema mgao wa kimya kimya, embu serikali itoe kauli Kama Kuna mgao tukanunue mishumaa, mficha malazi kifo umumbua
Duuh!! Moro nilikuwa naisifia, kumbe nako shida!! nimekaa sana hapo mkuu!!Morogoro imekuwa ni kawaida saana hata Jana huku nilipo wamekata kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 1 usiku na hata uliporud bdo ni baadhi ya maeneo
Umeme kwa huu mwezi unakatika Sana siku nzima, ukiuliza emergency wanajibu matengenezo, nimetembea mikoa Saba mwezi huu shida Ni hiyo hiyo, huku wengine wanasema mitambo imechakaa , huku wengine wanasema stigler, wengine wanasema mgao wa kimya kimya, embu serikali itoe kauli Kama Kuna mgao tukanunue mishumaa, mficha malazi kifo umumbua
Hao wengine huo umeme wanautoa wapi?.Tanesco wameshashindwa kuhudumia! Dawa ni kuruhusu makampuni mengine yaanze kusambaza umeme!!
Mkuu, maisha ya tz kila kitu tumeingiza siasa!! sikana kwamba vyavyo vya umeme havipo!!Hao wengine huo umeme wanautoa wapi?.
Hivi matangazo yenu kama haya huwa mnayaweka wapi hasa? Maana katika hizo social network ulizotaja sijaona tangazo la katazo la umeme.... Muwe update katika hizo social network zenu, kama mnataka kukata umeme mahali bas mtoe taarifa watu wajue.Tumetoa tangazo la matengenezo katika mashine zetu za kuzalisha umeme
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
DESEMBA 17, 2020
TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU, KINYEREZI II NA SONGAS.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna matengenezo katika Kituo cha Kufua Umeme kwa maji cha Kidatu na Vituo vya Kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Kinyerezi II na Songas.
Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti.
Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mashine zinatengemaa haraka.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.
Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100
Mitandao ya Kijamii :
Website:
www.tanesco.co.tz
Instagram: tanescoyetu
Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz,
Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu
Facebook: Tanesco Yetu
Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.