Hii hali ya watu kunuka mdomo na jasho ni ugonjwa au ni uchafu


Mimi nimekaa na wachina dah mkuu zile nguruwe zinanuka balaa, sijawahi kukas na race tofauti na hao wachina nione na wao kama wananuka.
 
kiumbe ambaye hapendezi akinuka ni mtoto wa kike tu,wanaume tuna mambo mengi sana kunuka ni kawaida.

tatizo linaanza hapa wewe mwanaume mwenzetu unapokwazika na harufu hizo.
hatuwezi kunukia masaa yote.
 
Dawa nyingi za meno ni fake..hapa wakulaumiwa ni tbs yetu..

Kuhusu mwili kunuka ni uchumi labda wengi wanashindwa kumudu kununua perfume..

na pengine kutokujali tu.. Kuna watu wao wapowapo tu ni wachafu by nature..
 
Mvua imenyesha ya kutosha jana na leo huko Dar. Muanze kuoga sasa wale mliokuwa mmeenda likizo ya kuoga japo mara mbili kwa siku kwa sababu ya uhaba wa maji.
 
Bila shaka huu uzi una mahusiano na Ile Pilau ya IFM,
 
Kuhusu kunuka mdomo(kutoa hewa yenye harufu mbaya) kunaweza kusababishwa na vitu vifuatavyo.
1. Uchafu ulioganda kwenye meno(mabaki ya vyakula)
2. Maambukizi kwenye kinywa (meno na fizi)
3. Maambukizi kwenye Koo na pua.
4. Maambukizi ya bakteria wa vidonda vya tumbo na
5. Kutosafisha kinywa na ulimi kwa umakini.
Kuhusu kunuka jasho,inaweza kusababishwa na mambo yafuatayo.
1. Hali ya hewa ya joto
2. Hulka ya Moto( mwili wenye asili ya kutoa jasho lenye harufu Kali au kunukuka kikwapa hata Kama Hali ya hewa so ya joto)
3. Kutokujisafisha vizuri hasa maeneo yaliyojificha.
4. Kutooga Mara kwa Mara
Mtu anapojigundua kuwa ana tatizo hasa la kunuka mdomo hupoteza ujasiri na huanza kujitenga na watu. Kupona tatizo hilo hutegemea na chanzo chake. Waone wataalumu wa afya
 
Waswahili Wana msemo wao unasema.
LAKE MTU HALIMTAPISHI.
inawezekana hata wewe unanuka ila kwa kuwa NI wewe mwenyewe unaona poa.
Ndivyo kwa BINADAMU wote tulivyo.utamuona mwenzio ananuka ila harufu yako utaichukulia poa.
Hakuna kitu kama hicho watu waache uchafu aisee....! Mtu unakuta akicheka meno yamejaa ukungu, ulimi una utandu mweupee, makucha marefu yamejaa uchafu, mtu kama huyo unamteteaje? Tuache uchafu asee
 
Kunuka mdomo na kutoa harufu Kali ya jasho ni ugonjwa kama magonjwa mengine.ila wakati mwingine kutozingatia usafi wa kinywa na kuoga walau mbili kwa siku husababisha hali hiyo pia.
 
Vile vimavi vya ulimwengu wa roho vipi? Kila ukiingia mahali penye watu wengi harufu ya yai lililooza inasikika. Au unafuatwa mara kwa mara na wale mainzi makubwa ya chooni. Unajitahidi sana katika usafi ila yote hayo unayo.
 
Vile vimavi vya ulimwengu wa roho vipi? Kila ukiingia mahali penye watu wengi harufu ya yai lililooza inasikika. Au unafuatwa mara kwa mara na wale mainzi makubwa ya chooni. Unajitahidi sana katika usafi ila yote hayo unayo.
naomba ufafanuzi
 
Reactions: THT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…