Hii hali ya watu kunuka mdomo na jasho ni ugonjwa au ni uchafu

Hakuna kitu kama hicho watu waache uchafu aisee....! Mtu unakuta akicheka meno yamejaa ukungu, ulimi una utandu mweupee, makucha marefu yamejaa uchafu, mtu kama huyo unamteteaje? Tuache uchafu asee
Ungekuwa msafi usingekuwa unaenda chooni na maji
 

sababu kubwa ya kunuka jasho ni kuwa wengi wa watanzania hawana usafiri wao wengi hutembea kwa miguu na anapofika ofisini anakuwa amelowa na jasho linatoa harufu ila yeye hawezi kulitambua na pia ulaji wa kitunguu swaum kitunguu maji husababisha harufu ya mwili. kwa kunuka mdomo sababu kubwa mtu kupiga mswaki bila dawa hii ina sababisha kutoa harufu hii kipato inachangia pili dawa ya meno nyingi feki unaweza ukapiga na dawa baada ya nusu saa ukajihisi kama hujapiga mswaki tatu kukaa mda mrefu bila kuongea au kutia kitu mdomoni husababisha harufu, wanawake wengi ni wajanja hupenda kutumia chiwing gum ya kutafuna (ubani wa kutafuna ) ili kupoteza harufu ukimuona mwanamke anatumia sana ubani ya kutafuna ujue mvivu kupiga mswaki
 
Watu hawali matunda ya kutosha ili kusaidia mchakato wa ndani ya mwili,wanakunywa maji kidogo. Pia muhimu mtu kutumia deodorant kwapani badala yake watu wanatumia body spray kwapani
 
Tatizo la kunuka mdomo shida itakuwa ni cement kwenye meno,nenda kasafishe hospital.
Ni ngumu Sana kwa watu kukuambia unanuka mdomo au kwapa
 
Watu hawali matunda ya kutosha ili kusaidia mchakato wa ndani ya mwili,wanakunywa maji kidogo. Pia muhimu mtu kutumia deodorant kwapani badala yake watu wanatumia body spray kwapani
Hata sabuni ukipaka kwapani harufu haitoki
 
Ni dalili ya sumu kujaatmwilini !hasa utumbo mpana au kitaalamu RECTUM !!Mabaki ya chakula yaliyo chacha huliwa na Bacteria kisha Bacteria hao hutoa uchafu uitwao tindikali unaonuka hasa gesi ya Sulphur dioxide!!!Harufu hiyo hutoka kwenye Rectum hadi mdomoni!!Ulaji wa vyakula vya kukoboa husababisha kinyesi kuganda tumboni na kushindwa kupata haja kubwa kutwa mara mbili au tatu hii huleta ugandaji wa uchafu kwenye Rectum!!hata jasho hunuka pia mbali na mdomo!!!
 
Ufafanuzi, "unalogwa unakuwa ni mtu wa kunuka tu" Kuna Binti alilogwa kila akiingia kwenye daladala watu wanashika pua. Amini usiamini, huo ndio ulimwengu wa roho, yakikupata utaamini. Kumbuka watu ni wengi ila binadamu ni wachache.
Duh
 
Kama wewe ni wakike sawa ila kama ni gentleman ulipaswa umwambie mlengwa kuliko hiki umefanya ni umama.

Kuna dogo alikuja kufanya field alikuwa na tatizo kama ulilosema nili mface akanieleza shida nikichogundua niuchumi ndo ilikuwa tatizo lililopelekea kurudia nguo mfululizo na viatu kupelekea kutoa harufu.
 
Waswahili Wana msemo wao unasema.
LAKE MTU HALIMTAPISHI.
inawezekana hata wewe unanuka ila kwa kuwa NI wewe mwenyewe unaona poa.
Ndivyo kwa BINADAMU wote tulivyo.utamuona mwenzio ananuka ila harufu yako utaichukulia poa.

Mmh
 
Mimi nahic ni kukaa muda mrefu bila kulaa...hili la kunuka mwli nafikir wataalam watakuja kulitolea ufafanuzi..ila yote tisa kumi binadamu wote tunanuku sema tumetofautiana tu viwango

Mtu anakula akikaa dakka kum hal inarud vle vle
 
Watu wanaoga sana na kupiga mswaki sana ila hizi ni sababu kuu kwa utafiti wangu.

1. Dawa za meno ndo chanzo cha kunuka midomo.

2. Chakula na vinywaji mtu alavyo ndo pia huchangia kunuka mwili.
Imeisha hiyo.

Kwahyo dawa nzuri ya meno ni ipi kwa faida ya weng
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…