Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Damas Ndumbaro amefanya uteuzi wa Kamati itayohusika kuratibu Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kwa mwaka 2023-2024.
Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kupitia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Kedmon Mapana limetoa baraka zake leo kwa kamati hiyo mpya ambayo BASATA imesema imeshaanza kazi.
Kamati hii inaongozwa na Mwenyekiti David Minja, Makamu Mwenyekiti Christine Mosha, Katibu Mrisho M.Mrisho na Wajumbe ambao ni Producer P Funk, Chris Torline na Natasha Stambuli.
Hapo kwa P funk kama judge patakuwa na mgongano wa maslahi..., manake huyo ni babake Paula wa Kajala!! Asaa si tuzo zote atampa mkwelima wake HARMONIZE??!! Au yule mwengine alokuwa wasafi , Rayvan?!