Hii Hapa Kamati ya Kuratibu Tuzo za Muziki Tanzania (TMA), P Funk, Seven Mosha Ndani

Hii Hapa Kamati ya Kuratibu Tuzo za Muziki Tanzania (TMA), P Funk, Seven Mosha Ndani

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Damas Ndumbaro amefanya uteuzi wa Kamati itayohusika kuratibu Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kwa mwaka 2023-2024.

Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kupitia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Kedmon Mapana limetoa baraka zake leo kwa kamati hiyo mpya ambayo BASATA imesema imeshaanza kazi.

Kamati hii inaongozwa na Mwenyekiti David Minja, Makamu Mwenyekiti Christine Mosha, Katibu Mrisho M.Mrisho na Wajumbe ambao ni Producer P Funk, Chris Torline na Natasha Stambuli.


View: https://www.instagram.com/p/Cz3SacsiSme/
 
Sijui sana haya mambo.lakini kwanini P funk apewe ujumbe sio uenyekiti ? Na hao wengine wengi hawafahamiki. Nilitegemea kukuta producers tu hapo
 
Learned brother, formerly waziri wa sheria, sasa anaongea ngoma! Nchi hii bwana!
 
Hapo kwa P funk kama judge patakuwa na mgongano wa maslahi..., manake huyo ni babake Paula wa Kajala!! Asaa si tuzo zote atampa mkwelima wake HARMONIZE??!! Au yule mwengine alokuwa wasafi , Rayvan?!
 
Back
Top Bottom