Hii hapa mikoa 12 inayoendesha uchumi wa nchi, inamiliki na kushikilia asilimia 70% ya uchumi wa Tanzania

Tujenge kituo Cha uwekezaji Kigoma au Tabora kutarget soko la DRC, RWANDA, BURUNDI na Zambia, badala ya nchi hizo kufuata mizigo China ziichukulie Tabora au Kigoma.
 
Mikoa isiyo na rasilimali kwa wingi itakuwaje ?
 
Kama hiyo mikoa ina mapato hayo ,mbona tunakopa sana ?
 
Hivi Dar es salaam itakuja kupitwa kiuchumia na mkoa mwingine?

Nawaza Tu.
 
Hivi Dar es salaam itakuja kupitwa kiuchumia na mkoa mwingine?

Nawaza Tu.
Sio rahisi na kiufupi haiwezekani.

Athari za ukoloni na Serikali.Kinachowesekana ni kupunguza dominance yake tuu sio kupitwa.

Endapo Makao Makuu ya Nchi yangekuwa Dodoma Toka awali ndio Ungekuwa Jiji kuu kama Nairobi,Tehran na kina Dar wangekuwa Miji ya Bandari tuu kama Mombasa nk.
 
Tujenge kituo Cha uwekezaji Kigoma au Tabora kutarget soko la DRC, RWANDA, BURUNDI na Zambia, badala ya nchi hizo kufuata mizigo China ziichukulie Tabora au Kigoma.
Kigoma inafunguka, point hapo ni miundombinu ijengwe kigoma, Tabora tayari ina shughuli nyingi za kiuchumi, kigoma ilikua sawa na kagera lakini naona kagera inaachwa hadi na kigoma sijui ule mkoa una laana gani maana wanakila kitu cha kufanya waendelee
 
Tanga sio ya kuona, Tanga iliwahi kua na viwanda vingi nyuma huko kuliko hata Dar, ona bandari ikiboreshwa, bomba la mafuta ya uganda likamilike, ile ni strategic zone toka enzi ya mkoloni
Reli ya Tanga-Arusha-Musoma na barabara plus Bomba zitasaidia ku push uchumi wa Tanga na uwekezaji wa viwanda ila inaweza kupita Mikoa yote lakini haitakuja kuipita Mwanza.

Inatakiwa uwapite Wabishi wa Mbeya,Moja ya Mkoa wenye watu aggressive kwenye Uchumi.

Takwimu za mwakani inaweza kuwa Juu ya Arusha.
 
Ni sahihi kabisa lakini hao watu walishaachana na masuala ya takwimu za NBS kwa maana hata wanaozijadili wamejikita katika kuongelea umasikini kwa kuangalia GDP ambayo hata hawajui inatafutwa namna gani na inachangiwa na nini na kuacha nini. Wengine wanajadili kwa kuongozwa na ukabila.

Kuna kitu wengi hawakielewi kuhusu kutengwa kwa makusudi kwa huo mkoa na ukiwa mfuatiliaji kwa kina utalijua hili. Achana na masuala ya kupelekewa meli inayobeba mizigo ambayo serikali haijui inazalishwaje kwa maana sehemu zingine utasikia Serikali imepeleka pembejeo za kilimo kwa wakulima lakini hutasikia kitu cha namna hiyo kwa mkulima wa eneo hilo.

Juzi bungeni kuna mbunge wa huko aliongelea masuala ya NIDA na uhamiaji na akaomba serikali ipeleke maafisa wanaofahamu kwa undani kuhusu hayo maeneo na wale ambao ni eneo geni kwao basi wawe informed na trained ipasavyo kuhusu hilo eneo. Ukiliangalia hili kwa macho ya juu utaona halina maana kwamba mbona maeneo mengine wanaenda tu lakini kwa upande wa mfanyabiashara au mwekezaji ataelewa ni kwanini huyo mbunge aliomba hilo. Nillilima huko miaka kadhaa najua ni kipi wanakumbana nacho sababu nilikumbana nacho mimi nikiwa nimepokelewa vyema na wenyeji.

Ni wazalishaji hodari wa Kahawa lakini jiulize serikali inaweka nini zaidi ya hapa juzi kuja na habari za kupunguza kodi sijui 15 na wakati huo huo unamzuia mtu asiuze kahawa yake sehemu nyingine ambako anapata bei kubwa zaidi kuliko anayoipata hata baada ya kuondoa hizo kodi 15. Ukiuza kwa aliyekuja kutoka nje ya nchi unaambiwa umeuza magendo wakati huo huo yapo maeneo mnunuzi kutoka kenya anaingia mpaka shambani ndani ndani huko bila shida yoyote. Je, hiyo GDP itapandishwaje?

Nilipata mashamba huko maeneo ya Karagwe kama unaenda eneo wanaita chabalisa na mpaka sasa niliyatelekeza yapata miaka 6 na kurudi kwetu kufanya mambo mengine. Sababu ya kuyaacha ni kile kinachoendelea kimya kimya kuhusu hilo eneo. Hivyo hali ya huko naijua vyema hasa katika suala zima la uzalishaji. Achana na ngonjera za mitandaoni sijui wenyeji hawapendi wageni, sijui hawapendi kazi ngumu na blaa blaa nyingi na hizo takwimu za NBS ambazo mtu anayepata mahitaji yake ya chakula cha kila siku kutoka shambani kwake moja kwa moja huku akihitajika kununua vitu vichache sana ambavyo hapati shambani anahesabiwa sawa na yule anayefanya spending ya kila kitu kwa kununua tena kila siku.

Ukiuliza kuhusu viwanda vya samaki vilivyokuwepo utakachojibiwa utaelewa. Kuna kiwanda cha kinaprocess kuuza kahawa ya kopo ya TANICA kama ilivyo AfriCafe. Ukiuliza kuhusu mikakakati ya serikali kukiwezesha zaidi ili kiprocess kwa wingi kahawa inayozalishwa huko utabaki unashangaa.

Achana na masuala ya kupanua bandari, kujenga barabara ya njia nne mjini ilhali bidhaa zinakotoka hakuna lolote linalofanyika. Watafute wenyeji na walioko kwenye mifumo ya serikali watakufumbua macho. Wewe hujawahi kujiuliza ni kwa nini Mkoa wa Kagera huwa hautajwi sehemu yoyote kila ikitamkwa mipango na mikakati kwenye mikoa ya kanda ya ziwa? Zaidi utasikia ukitajwa pale kunapolipuka magonjwa yanayoanzia nchi jirani na kebehi kadha wa kadha.

Kuna kipindi Rais Samia alifanya ziara huko na kuelezea mikakati kadhaa lakini jiulize ni kwanini katika kutembelea na kuzindua miradi mikubwa ya kiserikali inayotekelezwa Mkoani humo aliishia kutembelea kiwanda cha Kagera Sugar ambacho kila kiongozi akienda huko akiwemo PM wote wanatembelea hapo tu?

Ulishawahi jiuliza ni kwanini vyuo tuite colleges zilizofunguliwa huko miaka utawala wa JK zilifungwa miaka ya utawala wa JPM na mpaka sasa hazijafunguliwa wakati colleges zenye hadhi sawa na hizo zinaendelea kushamiri kwenye mikoa mingine? Kipindi cha JK alianza taratibu jitihada za kufufua fua baadhi ya sekta lakini alivyoondoka zikaanza kurudishwa na kupotezewa.

Uliwahi kujiuliza kwamba ni kwanini hata zikiwa zinasomwa taarifa kuhusu eneo la kanda ya ziwa itatajwa Mwanza, Mara, Geita na utaambiwa imepakana na Kigoma au Simiyu lakini hutasikia Mkoa wa Kagera ukitajwa?

Hao watu wanapambana wao kama wao na ndiyo maana kwa kiasi kikubwa wanatudharau sisi watu tulio katika maeneo mengine ambao tunapata support kubwa sana ya serikali lakini bado tunalia wakati wao wanapambana wenyewe kama wenyewe na wanasonga.
 
Reli ya Tanga-Arusha-Musoma na barabara plus Bomba zitasaidia ku push uchumi wa Tanga na uwekezaji wa viwanda ila inaweza kupita Mikoa yote lakini haitakuja kuipita Mwanza.

Takwimu za mwakani inaweza kuwa Juu ya Arusha.
Mwanza kuipita haiwezekani, ina uchumi mkubwa Kwa sasa uchimbaji wa dhahabu umetamalaki
 
Mwanza kuipita haiwezekani, ina uchumi mkubwa Kwa sasa uchimbaji wa dhahabu umetamalaki
Dhahabu hazichimbwi Mwanza,mgodi wanaoutegemea Kama ukianza ni ule wa Nyanzaga but ligtime yake itakuwa chini ya miaka 15.

Mwanza inategemea service industry,uvuvi na Mikoa inayoizunguka.

Nyie Tanga hakikisheni mnawashusha Wabishi Mbeya ndio nitajua mko seriously otherwise Viongozi wenu eti Wana Mpango wa kugawanya huo Mkoa so mtazidi kudidimia 😁😁

Tanga
 
Umejipinda kweli kweli ila inakuaje Mkoa wenye wasomi udai kwamba unatengwa? Si Kila Idara ya serikali mumejaa? Why msijipakulie minyama?

Visingizio fc 🤪🤪🤪🤪
 
Kwa Kigoma ni Suala la mda tuu itafunguka,hata kilichowasaidia Tabora ni kuimarika Kwa Barabara zote kuu zinazoingia na kutoka ndio maana imeanza kujitokeza maana ni Kwa mara ya kwanza Tabora inatokea kwenye list.

Miradi inayoendelea Kigoma ni Mingi sana ila poleni watu wa Tabora mnaenda kugawanywa so mtazidi kurudi kule kule kwenye level zenu za umaskini 🤣🤣
 
Umeandika kwa uchungu mpaka "nineogopa".

Pole sana mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…