Hii hapa ndio Timu Mpya ya uongozi wa Chadema Kitaifa

Hii hapa ndio Timu Mpya ya uongozi wa Chadema Kitaifa

Timu ya malofa watupu
Hawataweza ipeleka Chadema popote hao

Timu yote hakuna tajiri hata mmoja
Chama cha kwanza cha siasa cha malofa kilikuwa ni TANU mzazi wa CCM.

Kutokana na ulofa wao ndiyo maana waliweka zamu za kupeleka chakula kwa Mwalimu.

Kama unaiona CHADEMA ni chama cha malofa,jua hiyo ni dalili ya kuwa chama cha ukombozi. Maana vyama vyote vya kiukombozi huwa ni vyama vya malofa.
 
SIIPENDI, ALL ARE POWER MONGERS OF THE HIGHEST DEGREE PARTICULARLY, MWENYEKTI......ALIMBAGAZA, ALIMTUKANA, ALIMKEBEHI, ALIMDHALILISHA MBOWE SANA.
Joyce Mukya tuliza mshono mbona Mr. wako mwenyewe amekubali yaishe, utateseka sana mwaka huu.
 
Hapo viongozi ni Golugwa na Mnyika tu. Hao wengine ni virusi ndani ya CHADEMA na maadui wa demokrasia.
 
Hii Tumeileta kwa ajili ya Kuweka Kumbukumbu sawa kwa Wadau wa JF na Wengineo

View attachment 3224699

Mungu Ibariki Chadema
MKATABA MWINGINE BANDARINI NA MISRI WAZUA TAHARUKI YA CHINI KWA CHINI!

Ndugu Watanzania!
Tumepata taarifa kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Chuo cha Arab Academy for Science Technology and Maritime Transport (AASTMT) cha Misri wametia sahihi makubaliano ya kushirikiana kutoa mafunzo ya shughuli za kibandari kwa Wafanyakazi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo,makubaliano hayo, Tanzania kupitia TPA itapeleka watumishi wake kusoma Misri. Hii haitakuwa scholarships, bali Tanzania itakuwa ikilipia watu wake ada. Hata hivyo, makubaliano hayo yamezua mjadajala mzito miongoni mwa wadau ambao ni pamoja na manahodha wa meli, wahandisi wa meli na wahadhiri katika Chuo cha Ubaharia Tanzania yaanjli Dar es Salaam Maritime Institute (DMI) ambacho hutoa kozi hizo wakidai kuwa hiyo ni njia ya kukihujumu Chuo hicho. Baadhi ya hoja zao ni hizi:

Matumizi mabaya ya Fedha: Kutuma watumishi nje ya nchi kutagharimu fedha nyingi ambazo zingeweza kuwekezwa katika Chuo cha DMI ili kukiimarisha zaidi.

Kudhoofisha na kudhalilisha vyuo vya ndani: Hatua hiyo itaidhoofisha DMI na kufifisha zaidi ukuaji wake.

Kutelekeza Uchumi wa Blue: Kuimarisha vyuo vya ndani kunaiweka vizuri Tanzania katika kuinua rasilimali za Baharini.

Kukosekana kwa uwazi wa mchakato huo: Kwa kuwa mchakato huo haukuwa wa wazi, kuna maswali kuhusu kama uamuzi huo umebeba manufaa ya umma au una manufaa binafsi.
Wadau wanapendekeza kuwa:

TPA iwekeze zaidi katika Chuo chetu cha DMI kwa kuboresha na kuimarisha mitaala na kama itawezekana kuwaalika wakufunzi kutoka nje ya nchi ili kushusha gharama za Tanzania kupeleka watumishi wake nje. Njia nyingine ni kupeleka kusomesha wahadhiri kwa kozi ambazo hazipo nchini ili wakirudi waanzishe kozi hizo hapa Chuoni kwetu au pia kusomesha wahadhiri nje kwa kozi za PhD.

Wadau wanashangaa uamuzi wa TPA kupeleka vijana kusoma Uhandisi wa Meli nchini Misri wakati DMI ipo na inaheshimika sana hata nchi za Afrika Magharibi wanataka kuja kusoma DMI lakknky TPA wanaona Chuo hiki hakina maana.

Hata hivyo, kwa kuwa wadau hao wengi wao ni waajiriwa wa Serikali wanaogopa kujadiliana kwa uhuru na uwazi huku wengi wakitumiana ujumbe wa maandishi hata kupigiana simu.
Sisi Askofu Mwamakula tulipopata taarifa hizi kupitia kwa mmoja wa wastaafu tumeona ya kuwa ni vizuri tuweke hadharani jambo hili ili kuwapa uhuru wadau kuliweka andiko hili huko katika makundi yao sogozi.

Pamoja na hayo, kwa kuwa baadhi wamehoji juu ya uwazi wa mchakato huo makubaliano hayo, tunashauri mchakato huo uchunguzwe kama ulikidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kuhusu masuala ya mikataba na nchi au taasisi za kimataifa. Je, kama wadau wakuu wanahoji makubaliano hayo, ni nani aliyeshiriki katika kushauri juu ya jambo hilo?

Je, kulikuwa na ushirikishwaji wowote? Ni nani alihusika kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu hili? Je, kuna shida gani ilijitokeza katika Chuo chetu cha DMI hadi tuingie mikataba ya kutaka kusomesha watumishi katika fani ambazo zipo DMI? Je, mkataba unaeleza ni fani gani na kwa ngazi gani za kusomesha watu kule Misri? Je, mkataba huo unatoa kipindi cha muda gani? Je, mkataba huo unaweza kuwekwa hadharani kwa wadau ili waweze kuusoma na kuuelewa?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Februari 2025; saa 5:20 usiku
 
Back
Top Bottom