Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Ule mtego hata wewe hauchomoki.
Pia ubahili.
Ila muda sio mrefu naachana nayo.sitaki kuuza kabla sijanunua mpya.maana kuna wakati mitego inagoma kufyatuka.
Nimejifunza kitu kimoja katika maisha cheap ni ghali

Kwenye miaka ya 2014 nilinunua samsung nchi 43 kwa 1.5 sikujutia,ilikaa miaka saba bila shida yoyote,baadae ikakaa mwaka mmoja bila kuwashwa ndio kuna kitu kilizingua ni bei ndogo tu,lkn ipo store imepumzika
 
Nitumie huo unyama mwana...hii hisense imenizoea sasa 4 yrs na bado iko poa
Au uchukue hii Samsung 55"
20240919_131451.jpg
20240919_131256.jpg
20240919_131454.jpg
 
Anasema tangu anunue Iko hivo labda afanye hivo
Kwahiyo wez walisubir mtengeneze
Ya bimkubwa ilikuwa safi kabisa,ila ilikaa kama miezi sita bila kuwashwa ndo kuja kuwashwa ikawa dark,unajua hivi vitu vikianza kutumika usiache kabisa kuviwasha washa

We acha tu kpnz,baada ya kutoka kwa fundi kama mwezi mmoja wezi wakaona isiwe tabu ngoja wakajiachie na smart tv
 
Kila mtu anapenda kumiliki kitu kizuri ila baadhi kipato hakiruhusu, hii imepelekea kuwepo kwa bidhaa za kila aina sokoni ili kubeba pesa yoyote mteja aliyonayo. Kwa upande wa TV zipo kampuni nyingi sana na hapa nazigawa kwenye makundi matatu

1. Samsung LG SONY Panasonic
2. TCL Hisense Haier
3. Alitop Aborder Ailyons Solarmax Skyworth Mr.UK Mewe Boss e.t.c

Kutoka kundi namba moja TV ambazo zimezoeleka sana ni LG na Samsung, tofauti ya hawa wawili LG anakupa picha kali (real 4K) wakati Samsung anakupa picha kali pamoja na frame kali kuliko frame ya LG. LG anakupa durability na kioo chake ni kigumu kupasuka kuliko Samsung.

LG wanakupa series 4 ambazo ni (UHD NANOCELL QNED OLED) Samsung wao wana (UHD QLED OLED)

Bei zake zinapanda kulingana na latest series, kumiliki TV za kundi hili lazima uwe una pesa kulingana na series unayotaka pamoja na inches ngapi unahitaji na ndio TV zenye bei kubwa zaidi sokoni.

Namba mbili tukianza na TCL ni TV nzuri ambayo kama unapenda kitu kizuri na umeshindwa kufika bei ya hapo juu, TCL wanakupa picha nzuri pia inadumu ukiweka ndani ni mkataba.

Tukija kwenye hisense wenyewe wana series za bei ndogo na kubwa, hawa jamaa wana TV nzuri kulingana na bei zao ila quality yake haiwafikii hao wazee hapo juu, pia ndio TV ambazo zinauza sana sokoni kwa sasa kutokana na jina lakini pia bei zao zinaendana na watu wa uchumi wa kati, hawa jamaa baadhi ya series zao zinarudi sana kwa fundi ila ukiotea ni mkataba.

Haier wenyewe wamekuja karibuni kwenye soko la Tanzania na wanafanya vizuri, bei zao zipo chini kidogo ya Hisense, ukikosa pesa ya kununua hisense basi kimbilia hapa kabla hujafika namba tatu kwa wachina wenyewe.

Kundi namba tatu nimeweka kampuni za kichina zilizojaa sokoni, hawa wameamua kumuuliza mteja ana bei gani kisha watengeneze bidhaa, kwa hili kundi TV yenye picha nzuri ni Alitop na Skyworth lakini pia bei zao ni nzuri unaweza kumiliki 43" below 450k price; Aborder wanakupa durability nzuri pia.

Uliza swali lolote kwenye coments kulingana na mada, ukitaka kujua bei weka kampuni gani na inches ngapi, lakini pia series kama haufahamu uliza nitajibu.
Ciao
Napenda Sana Sony Tv hua naona picha inakua nzuri,vp uhalisia wa hili la ubora wa picha ukilinganisha na samsum na Lg?Vp pia kuhusu uimara wake bw koffi annan?
 
Back
Top Bottom