Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Acha uongo aisee nina freezer la Life is good mwaka wa 10 huu linadunda tu sema itakua unanunua vile vilivyopachikwa nembo ya LG sio LG yenyewe wewe ndio mtu wa kwanza naona unaiponda LG..
Acha ujinga, sio vifaa vya Kampuni yote wala hakuna sehemu yoyote niliposema vyote ni vibovu, hapa tunaongelea TV, ni wapi nimeongelea vifaa vyengine vya LG kuwa ni vibovu?
 
Acha uongo aisee nina freezer la Life is good mwaka wa 10 huu linadunda tu sema itakua unanunua vile vilivyopachikwa nembo ya LG sio LG yenyewe wewe ndio mtu wa kwanza naona unaiponda LG..
Msome na mwelewe mtu anapokuwa anaelezea, hakuna sehemu niliposema product nyingine za LG kuwa ni mbovu zaidi ya TV, kiufupi nimeongelea TV. Acha uongo.
 
Msome na mwelewe mtu anapokuwa anaelezea, hakuna sehemu niliposema product nyingine za LG kuwa ni mbovu zaidi ya TV, kiufupi nimeongelea TV. Acha uongo.
LG TV hazina shida unatumia zile za uongo mazee...
Samsung ya rand 17,000 LG utaikuta ipo rand 26,000 na hawana promotion wala sell na bidhaa zao zinaisha hapo kwenye duka la jumla..
Anaengoza kwa ubora ni Sony, LG na Samsung wanalingana anakuja Skyworth anafata Hisence..
 
Vitu vya Electonics tunanunua chimbo moja Jhb hapo
20240920_113113.jpg
20240920_112358.jpg
20240920_113105.jpg
 

Attachments

  • 20240919_123422.jpg
    20240919_123422.jpg
    577.4 KB · Views: 16
Kila mtu anapenda kumiliki kitu kizuri ila baadhi kipato hakiruhusu, hii imepelekea kuwepo kwa bidhaa za kila aina sokoni ili kubeba pesa yoyote mteja aliyonayo. Kwa upande wa TV zipo kampuni nyingi sana na hapa nazigawa kwenye makundi matatu

1. Samsung LG SONY Panasonic
2. TCL Hisense Haier
3. Alitop Aborder Ailyons Solarmax Skyworth Mr.UK Mewe Boss e.t.c

Kutoka kundi namba moja TV ambazo zimezoeleka sana ni LG na Samsung, tofauti ya hawa wawili LG anakupa picha kali (real 4K) wakati Samsung anakupa picha kali pamoja na frame kali kuliko frame ya LG. LG anakupa durability na kioo chake ni kigumu kupasuka kuliko Samsung.

LG wanakupa series 4 ambazo ni (UHD NANOCELL QNED OLED) Samsung wao wana (UHD QLED OLED)

Bei zake zinapanda kulingana na latest series, kumiliki TV za kundi hili lazima uwe una pesa kulingana na series unayotaka pamoja na inches ngapi unahitaji na ndio TV zenye bei kubwa zaidi sokoni.

Namba mbili tukianza na TCL ni TV nzuri ambayo kama unapenda kitu kizuri na umeshindwa kufika bei ya hapo juu, TCL wanakupa picha nzuri pia inadumu ukiweka ndani ni mkataba.

Tukija kwenye hisense wenyewe wana series za bei ndogo na kubwa, hawa jamaa wana TV nzuri kulingana na bei zao ila quality yake haiwafikii hao wazee hapo juu, pia ndio TV ambazo zinauza sana sokoni kwa sasa kutokana na jina lakini pia bei zao zinaendana na watu wa uchumi wa kati, hawa jamaa baadhi ya series zao zinarudi sana kwa fundi ila ukiotea ni mkataba.

Haier wenyewe wamekuja karibuni kwenye soko la Tanzania na wanafanya vizuri, bei zao zipo chini kidogo ya Hisense, ukikosa pesa ya kununua hisense basi kimbilia hapa kabla hujafika namba tatu kwa wachina wenyewe.

Kundi namba tatu nimeweka kampuni za kichina zilizojaa sokoni, hawa wameamua kumuuliza mteja ana bei gani kisha watengeneze bidhaa, kwa hili kundi TV yenye picha nzuri ni Alitop na Skyworth lakini pia bei zao ni nzuri unaweza kumiliki 43" below 450k price; Aborder wanakupa durability nzuri pia.

Uliza swali lolote kwenye coments kulingana na mada, ukitaka kujua bei weka kampuni gani na inches ngapi, lakini pia series kama haufahamu uliza nitajibu.
Ciao
TCL 55" 4K bei gani?
 
Back
Top Bottom