aziz habib
Member
- Mar 13, 2015
- 76
- 88
Nimekuwa kwenye hali nisiyoielewa kwa muda mrefu sasa. Yaani kila jambo nilifanyalo likikaribia kufanikiwa linaharibika.
Yaani naweza nikapata ramani ya pesa ila ikifikia hatua ya mwisho kuipata dili linaharibika katika hali isiyoeleweka na hata nilipofikia hatua ya kutumia msemo wa kimfaacho mtu chake kwa kutaka kuuza baadhi ya vitu ninavyomiliki hali inakuwa hivyo mteja akipatikana dakika ya mwisho anaingia mitini.
Kukopa nako unapata uhakika wa mkopo ikifikia hatua ya mwisho mambo yanabadilika. Waungwana naomba msaada wenu wa mawazo nijue wapi nakosea maana imefikia hata kodi ya pango najikuta napitisha na nikipata pesa ni kupunguza deni sio kumaliza.