Hii imekaaje? Kila nikikaribia kupata pesa mambo yanaharibika

Hii imekaaje? Kila nikikaribia kupata pesa mambo yanaharibika

Nimekuwa kwenye hali nisiyoielewa kwa muda mrefu sasa. Yaani kila jambo nilifanyalo likikaribia kufanikiwa linaharibika. Yaani naweza nikapata ramani ya pesa ila ikifikia hatua ya mwisho kuipata dili linaharibika katika hali isiyoeleweka na hata nilipofikia hatua ya kutumia msemo wa kimfaacho mtu chake kwa kutaka kuuza baadhi ya vitu ninavyomiliki hali inakuwa hivyo mteja akipatikana dakika ya mwisho anaingia mitini. Kukopa nako unapata uhakika wa mkopo ikifikia hatua ya mwisho mambo yanabadilika. Waungwana naomba msaada wenu wa mawazo nijue wapi nakosea maana imefikia hata kodi ya pango najikuta napitisha na nikipata pesa ni kupunguza deni sio kumaliza.
Tatizo lako unawaambiaga watu mipango yako...mipango ni siri
 
Kuna mtu mmoja aliniambia huenda kuna watu wamepiga pini harakati zangu kwa namna ya nguvu za giza ila mzazi wangu ananiambia nisiamini sana hizo kauli
Ni kweli usiamini...ni wakati bado tu
 
Tatizo lako unawaambiaga watu mipango yako...mipango ni siri
Hili nimeanza kulizingatia mkuu...ni kweli nilikuwa nawaamini baadhi ya watu na kuwapa baadhi ya mipango ya mambo niliyokusudia kufanya nikiamini vijana wenzangu hawawezi kuwa na roho hizo ila kuna mtu amenisanua kuwa huenda hao niliowahi kuwashirikisha mambo yangu wanaweza kuhusika kwa namna moja au nyingine
 
Pole sana hiyo Hali inataka kufanana na mm tofauti ni Kwamba mm Huwa dilinzangi Zina tiki kabisa, ila baada ya muda furani mambo Huwa yanaharibika vibaya mno, yaani Huwa inatokea msara mkubwa na kujikuta kile nilichokipata hukitumia Kwa ajili ya kutatua tatizo. Pole sana
 
Sometymz napata fungu linalotosha kukamilisha mambo mengi sana ila cha ajabu itatokea ishu ya kuharibu baadhi ya mambo yasitekelezeke
 
Back
Top Bottom