Hii imekaaje kudharau watumiaji wa simu za Tecno na Itel ilihali wote mnakuwa na access ya vitu vinavyofanana

Tecno, itel na infinix ni simu ila za kiwango cha chini.

Lazima tukubaliane kwamba kwenye maisha kuna viwango ama levels, hizi zinatokana na vitu vingi mojawapo ni ubora.

Mfano, unaweza kupanda toyo la miguu 3 kutoka Dar kwenda Dodoma, utafika tu sawa na Shabiby ingawa mtatofautiana muda wa kufika. Barabara mnapita moja ile ile lakini tofauti ya yoto ama guta na Shabiby iko wazi.

Wewe unaweza kua na paso mwingine ana range rover sports mnaenda Arusha kutokea Dar, yote ni magari na mtafika wote Arusha kwa nyakati tofauti lakini kuna vitu kama speed, comfortability, security, safety nk ndio vitatofautisha paso na range.

Kwenye simu iko hivyo hivyo. Tecno ni simu ila za viwango vya chini, choka mbaya. Vifaa vinavyotumika kutengeneza tecno ni vya ubora hafifu ama wa chini.

Tecno tunatumia tu kwa sababu ya umasikini ila tukiwa na hela tungetamani kutumia simu za maana kama Samsung, Iphone, Huawei, Vivo, Xiaomi, LG, Lenovo ama makampuni mengine ya maana.
 
Tecno n mdhamin wa Man City , kama hazitumik huko kwann wakadhamin club ya huko?
 
Natumia Infinix , nafanya graphics mwenyewe kila siku kwenye simu yangu (kwaajili ya biashara) hiyo canva , adobe etc zipo

Mna ujinga mwingi
 
Ubora au uwezo wa simu unapimwa kwa specifications sio mtazamo wako

Porojo nyingi
 
Hebu support hii na Data

Hakuna simu inayozima kwa kuwekewa mzigo mzito, unless ina miaka zaid ya minne au mitano ua matumiz
Siyo, Kweli!
Nimezitumia ITEL na TECNO sana.

Nilikuwa na ITEL mpya kabisa imetoka shop na hata miezi 5 bado ukiipiga mzigo mzito inazima.

Na TECNO hivyo hivyo niliinunua shop mpya kabisa nikichat sana hapa JF inazima.

Nikidownload files kubwa inazima au inakata network na haijamaliza miaka miwili.

Jamaa zangu wawili nao walipiga mchongo, Halafu wakaingia shop wote wakachukua ITEL mpya.

Lakini cha ajabu ITEL zao zinakata NETWORK kila wakipiga simu au wakishusha files na tuko mjini kati Rock City.

Tukairudisha dukani ITEL inayokata NETWORK mara kwa mara, Tukapewa nyingine mpya nayo ina 4G na tukaweka HALOTEL 4G lakini inasumbua sana kwenye kudownload, ni nzito, inapakua slow slow sana tofauti na Infinix, Samsung, Iphone, Smartphones zingine.

ITEL na TECNO zina SAR kubwa pia. Kwanini MCHINA hatumii TECNO kwao?
 
Hakuna anayemdharau mtumiaji wa TECNO au AITEL isipokua tunawatania Kama tunavyowatania wasukuma kwa ushamba walionao, au wangoni kwa kupenda pombe na wanawake, au wakinga kwa uchawi, au waha kwa uchafu na ubishi, au wapare kwa ubahili au waluguru kwa kuongea upupu au wakurya kwa tabia zao mbaya.
 
Ukishusha mzigo mzito zina jam, Zinazima.

Hazipakui High Quality Pure HD.

Zina viwango vikubwa vya SAR tofauti na zile za Ulaya na America.
Mzigo mzito wa tani ngapi? Na high quality pure HD ndo ipoje? Yawezekana mi mgeni kwenye ulimwengu wa teknolojia viwango vya SAR ndoa vinakuwaje?
 
Najua unaipenda tecno yako ila nakwambia tu hiyo ni upuuzi sio simu
 
Hivyo vitu mna uhakika navyo au mnaandika vitu vya kusadikika watu wameinstall apps za ukubwa tofauti na still simu inapiga mzigo kama kawaida
 
Wanaume wa Dar unapata 4 ya 28 unajisifu?
Umeunga unga elimu mpaka kinyaa
Sikia ndugu, soma std 7 faulu, soma f 1 hadi 4 faulu soma f 5 na 6 faulu nenda University. Kuunga unga ina maana shule wewe umelazimisha tu umetumia ujanja ujanja[emoji23][emoji23]
 
Mkuu umeumaliza kila kitu. Ishi unavyotaka wewe sio wanavyotaka walimwengu utakuwa mtumwa.
 
unachekesha sana.
nipe sababu ya kulinganisha majina na vitu.
bmw inamiaka mingapi na passo ina miaka mingapi
Kwa tafsiri hiyo ukiwa unamiliki bmw unakuwa na kibali cha kumdharau anayemiliki Passo kuna wakati tujifunze kuappreciate vitu vya watu.

Kuna mataasisi yenye wataalamu yanasimamia standard ya hivi vitu ukiona bidhaa imeingia sokoni ni wazi kuwa imekidhi viwango vilivyowekwa.

Sasa wewe unayejifanya mjuaji na akili zako za darasa la saba b unakomaa kuwa Tecno sio simu ilihali hata basics za kutengeneza calculator huzijui.
 
Ni mtu anayejiamini na mwenye akili hawezi kufanya kitu sababu ya kufurahisha watu au sababu ya kuogopa watu watakachosema wasiojitambua ndo anaweza kuwa na akili mbovu kiasi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…