Hii imekaaje kudharau watumiaji wa simu za Tecno na Itel ilihali wote mnakuwa na access ya vitu vinavyofanana

Hii imekaaje kudharau watumiaji wa simu za Tecno na Itel ilihali wote mnakuwa na access ya vitu vinavyofanana

Kivipi unafananisha basi na simu? Na kama class ndo inakufanya utumie simu fulani bila kuangalia specifications ni wazi unahitaji ukombozi wa kifikra.
Uko sahihi kabisa bro. Watu wengi wana UKIMWI wa Mawazo na kasumba iliyopitiliza.Kimsingi TECNO,ITEL,etc. Walifanya utafiti wa Mazingira ya Africa na zinafaa kwa Watu wanaotambua hilo. Wengi wanadanganyika kuhusu bei kumbe issue ni brand tu na gharama za uzalishaji lakini performance etc the same.
 
Unakuna pale unapoweza.

Kumekuwapo na imani kuwa watumiaji wa simu wa makampuni ya Tecno na Itel ni watu washamba na wasio na uwezo kifedha. Kiukweli katika mtizamo wa kutokuwa na uwezo kifedha naweza kuunga mkono lakini katika kuwa washamba ni jambo lisilo na ukweli.

Hivi inakuwaje mtu una akili zako timamu kabisa unaanza kumdiss mtu anayetumia Tecno au Itel wakati wote.

1. Mna access ya internet
2. Mnaweza pata kile mtakacho kama apps, muziki, videos na movies
3. Mna Ram na storage zinazofanana.
4. Camera yenye quality
5. Tunapost, tunacomment, tunashare na kulike.

Yawezekana utofauti upo kati ya makampuni aya na mengine lakini sio utofauti ule wa kuanza kukejeli na kudharau hizi simu.

Na kama ushamba ni yule anayemiliki simu ya gharama kubwa wakati angeweza kuwa na simu ya gharama nafuu lakini yenye performance kubwa.

Je simu ya gharama kubwa inayotumika kusikiliza muziki na kufuatilia maisha ya wasanii inaweza kulingana na simu ya gharama ndogo inayotumika kujisomea na kwenye biashara?

From northern part of Tanzania.
Unataka kusema mwenye itel naye anaingia app store kama kawaida?

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Ukweli utabaki pale pale
Africa ni jalala la mchina...
Ma-pikipiki
Ma-simu
Ma- nguo
Nk
Hapana.Usiongee hivyo Baba N. Mchina ana uwezo mkubwa wa kutengeneza vitu vyenye quality ila kwa utafiti wake amelenga masoko ya watu maskini na amefanikiwa kwa hilo. Hivyo kwa sasa hata kapuku unaweza kumiliki pikipiki au smartphone hayo ni maendeleo japo baadhi yetu tumetawaliwa na kasumba ya 🤷‍♂️ - wakati wote tunataka tupate sisi wengine wasipate. Mbaya hiyo.............
 
Nimewahi kumiliki Samsung AH 300 na Samsung j5 prime very expensive ila sijawahi kuona simu zinapata moto kama hizo hadi sometimes nikiwa bar namwomba mhudumu aniwekee kwenye fridge dk 10 (seriously) .
Pili hazikai na chaji halafu zina memory ndogo mwanga hafifu na ni SAMSUNG genuine made in Vietnam na Korea.
Nahudhuria sherehe watoto wana tecno zao wanarecord video ndefu ndefu gizani na zinatoka fresh mm samsung inalete giza tu shenzy nikaachana na huo ujinga nimeanza kutumia tecno hizi Pouvoir zina ubora zinakaa na chaji hadi chaja inapotea.
Kuna watu wana iphone original tunakaa sehemu zina poor signal reception simu zao hazipati mtandao ila tecno zinatamba tu.
Kuna baadhi ya Samsung ubora wake ni kwenye kusikiliza miziki tu.
 
Div four anasoma mpaka anapata Phd.

Endeleeni kukazana kudiss simu zetu pendwa wakati sisi tukiendelea kuenjoy digital life.
Ndo kama hivi wewe unainjoi lakini huku unalalama kuwa unadharauliwa... Hapo ulipo ukiidharau inayoheshimika hata wewe mwenyewe utajidharau... NDO TAABU UNAYOIPATA.. UKAVAE MAGUNIA SASA NA MAGOME YA MITI MAANA YOTE YANAFICHA UTUPU
 
Hazina ulinzi, nikiokota simu yako naweza kui fungua hata kama uliweka screen lock, kuna software kibao za computer kama dc unlock zinafanya hio kazi.

Processor zale nyingi ni kiwango cha chini, ni media tek

Hazijapitia kukaguliwa kwa usalama wa afya ili kupunguza gharama, ukaguzi wa simu unapandisha bei ya simu kwa kuwalipa wakaguzi.

Wanaiga, hawabuni ama kuvumbua vyao.
 
Huu uzi ni mahususi kwa sisi masikini kujifariji, sizitaki mbichi hizi...ila tungekuwa na kipato cha kutosha wengi wetu tungenunua hizo Samsung na iphone pro max[emoji205]
Hufikiri sawasawa, nadhani tatizo ni umri wa baadhi ya watu humu na majukumu yao.

Kwa mfano mimi inanigharimu wastani wa million 12 kwa mwaka kucover school fees za watoto(Siyo lazima iwe kweli) lakini simu yangu haizidi laki mbili, nina uwezo wa kununuwa simu ya aina yoyote ile lakini hayo niliyafanya wakati tunatumia Blackberry na majukumu hayakuwa makubwa.

Kwenye thread kama hizi ni rahisi sana kuwajuwa kula kulala ambao kwayo simu ndio kitu cha thamani anachomiliki.

By the way binafsi naichukia tu Tecno, ni chuki zangu tu binafsi.
 
Back
Top Bottom