Hii imekaaje kuhusu tathmini ya uharibifu wa shamba baada ya mifugo kuharibu shamba?

Hii imekaaje kuhusu tathmini ya uharibifu wa shamba baada ya mifugo kuharibu shamba?

Ozone star

Member
Joined
Aug 1, 2018
Posts
7
Reaction score
3
Kuna documents kutoka halmashauri ya wilaya fulani hivi. Inaelezea tathmini ya jinsi ya kutatua migogoro ya mifugo itakapoharibu kila aina ya mazao na malipo yake.

Mfano:
Ng'ombe wakiingia shamba la mahindi muda wowote wa ukuaji wa mazao hata kama mahindi yana wiki toka kupandwa, inapigwa hesabu yote toka kuandaa shamba kupanda, kupalia hadi mavuno. Mfano, Tsh 600,000/. Ni uendeshaji shamba.

Halafu inajumlishwa na mauzo ya mazao yote baada ya mavuno. Mfano, Mauzo ni Tsh 1,200,000/-. Hivyo 600,000+1,200,000= 1,800,000. Hivyo mwenye mifugo atatakiwa kumlipa mkulima 1,800,000/-Tshs.

Maswali:
Je, hapo haki imetendeka? Hii ni sheria ya nchi inayotumika hata mahakamani? Je, hizi kanuni zinazoletwa vijijini zilizotungwa na watu wachache huko halmashauri pia zipo mahakani? Inawezekana vipi gharama za uendeshaji zijumlishwe na mauzo ndo alipwe mkulima tena kwa umri wowote wa mazao?

Maoni/mawazo binafsi:

Ingetakiwa mfugaji auziwe mazao kwa tathmini tu kwamba kama angavuna?, Ingetoa gunia kadhaa zenye thamani ya Tsh 1,200,000/. Maana yake mkulima angepata faida ya Tsh 600,000/-

NB: Hii ni tathmini aliyoifanya bwana shamba leo na kumpa mkulima hesabu ya mfano huu alipwe au aende mahakamani.

Naomba wataalam wa sheria mnisaidie.
 
Kisheria hakuna ghalama za namna hiyo, isipokuwa wilaya wameweka ivo Ili kidhibiti uchungaji holela wa mifugo. Yaani ni sawa na ukute bango la faini ya sh 50,000 kwakosa la kupita na pikipiki kilabuni. Kiuhalisia ukibainika faini huwa ni zile zinazolipika. Iwapo mwananchi ataambiwa alipe Kwa mfumo aao na akigoma akifika mahakamani faini itaendana na uharibifu.
 
Hiyo imekaa vizuri sana itaepusha uzembe kwa wenye mifugo hakuna kitu kinauma kama umeandaa shamba lako umeweka na mipango yako na malengo halafu anatokea mzembe mmoja analisha mifugo yake kwa uzembe. Tena ilitakiwa faini iongezwe itasaidia umakini.
 
Hii kitu Huwa haina kanuni maalum, Kila sehemu ina utaratibu wake. Mara nyingi uhasama unaongezeka tu.
 
Back
Top Bottom